Vietnam Kaskazini : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 46 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q172640 (translate me)
Svg version (GlobalReplace v0.6.5)
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:LocationNorthVietnam.png|thumb||Mahali pa Vietnam Kaskazini 1955-1976]]
[[Picha:North Vietnam in its region.svg|thumb||Mahali pa Vietnam Kaskazini 1955-1976]]
[[Picha:NoordVietnamKaart.png|thumb||Ramani ya Vietnam Kaskazini 1955-1976]]
[[Picha:NoordVietnamKaart.png|thumb||Ramani ya Vietnam Kaskazini 1955-1976]]
[[Picha:Flag_of_Vietnam.svg|thumb||Bendera ya Vietnam Kaskazini 1955-1976]]
[[Picha:Flag_of_Vietnam.svg|thumb||Bendera ya Vietnam Kaskazini 1955-1976]]

Pitio la 20:26, 28 Oktoba 2018

Mahali pa Vietnam Kaskazini 1955-1976
Ramani ya Vietnam Kaskazini 1955-1976
Bendera ya Vietnam Kaskazini 1955-1976

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam au Vietnam Kaskazini ilikuwa jina la dola katika kaskazini ya Vietnam ya leo kati ya 1946 na 1976.

Jamhuri hii ilitangazwa na Ho Chi Minh baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mnamo tar. 2 Septemba 1945 mjini Hanoi katika kaskazini ya koloni ya Kifaransa ya Indochina. Tangazo lilijumlisha eneo la majimbo ya Tonking na Annan ya Indochina ya Kifaransa. Ho Chi Minh alikuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti kilichotawala harakati ya Viet Minh iliyoendesha upiganbaji dhidi ya Ufaransa.

Tangu 1946 Ufaransa iliyowahi kufukuzwa katika Vietnam na Wajapani wakati wa vita kuu ilijaribu kurudisha utawala wake. Katika vita ya Indochina jeshi la kikoloni la Ufaransa lilishindwa mwaka 1954 na Mkutano wa Geneva juu ya Indochina ya 1954 liligawa koloni ya awali katika nchi za Laos, Kambodia na Vietnam. Vietnam iligawiwa kwa sehemu mbili yaani Vietnam Kaskazini (rasmi: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam) na Vietnam Kusini (rasmi: Jamhuri ya Vietnam). Mapatano ya amani yalitarajia kuwepo kwa uchaguzi wa kitaifa lakini serikali ya kusini ilikataa kura hiyo.

Hivyo Vietnam Kaskazini ilibaki kama nchi ya kikomunisti na Ho Chi Minh alikuwa rais.

Tangu 1960 uongozi wa Vietnam Kaskazini uliamua kujenga harakati ya Vietkong katika Vietnam Kusini kwa shabaha ya kupindua serikali ya Kusini na kuunganisha nchi yote. Hii ilisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe ya kusini na kuingia kwa Marekani.

Kuanzia 1964 Vietnam Kaskazini ilituma wanajeshi wengi kwenda kusini waliofaulu kushinda vita na kuteka Saigon mwaka 1975 wakiunda serikali ya kikomunisti ya kusini. Mwaka 1976 sehemu zote mbili za Vietnam ziliunganishwa kwa jina la Jamhuri ya Kijamii ya Vietnam.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vietnam Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.