Angeline Mabula : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 16: Mstari 16:


== Maisha na elimu ==
== Maisha na elimu ==
Angelina Mabula alizaliwa [[tarehe]] 6 Mei 1962. Alisoma [[shule ya sekondari]] Lake na kuhitimu masomo yake [[mwaka]] [[1981]].
Angelina Mabula alizaliwa [[tarehe]] 6 Mei 1962. Alisoma [[shule]] ya [[sekondari]] Lake na kuhitimu masomo yake [[mwaka]] [[1981]].


Yeye ni [[mhasibu]] kwa [[taaluma]]. Mnamo [[1982]], alipata [[shahada]] ya [[cheti]] cha [[Uhasibu]]. Aliendelea kupata [[diploma]] ya juu na baadaye kuhitimu katika Uhasibu katika [[Taasisi ya Usimamizi wa Fedha]] mwaka [[1990]] na [[1991]] kwa mtiririko huo. Alipata uthibitisho wa wahasibu wa umma kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi mnamo mwaka [[2000]].
Yeye ni [[mhasibu]] kwa [[taaluma]]. Mnamo [[1982]], alipata [[shahada]] ya [[cheti]] cha [[Uhasibu]]. Aliendelea kupata [[diploma]] ya juu na baadaye kuhitimu katika Uhasibu katika [[Taasisi ya Usimamizi wa Fedha]] mwaka [[1990]] na [[1991]] kwa mtiririko huo. Alipata uthibitisho wa wahasibu wa umma kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi mnamo mwaka [[2000]].

Pitio la 02:29, 23 Oktoba 2018

Angelina Mabula
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanasiasa
Chama cha kisiasa Chama cha Mapinduzi

Angelina Mabula (amezaliwa 6 Mei 1962) ni mwanasiasa wa chama cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Yeye ni Naibu Waziri wa sasa wa maendeleo ya binadamu. Pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela.

Maisha na elimu

Angelina Mabula alizaliwa tarehe 6 Mei 1962. Alisoma shule ya sekondari Lake na kuhitimu masomo yake mwaka 1981.

Yeye ni mhasibu kwa taaluma. Mnamo 1982, alipata shahada ya cheti cha Uhasibu. Aliendelea kupata diploma ya juu na baadaye kuhitimu katika Uhasibu katika Taasisi ya Usimamizi wa Fedha mwaka 1990 na 1991 kwa mtiririko huo. Alipata uthibitisho wa wahasibu wa umma kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi mnamo mwaka 2000.

Aidha, alipata shahada ya ujuzi katika maendeleo ya jamii na kiuchumi kutoka Chuo Kikuu cha Open. Mabula alikuwa na kazi ya muda mrefu kama mkaguzi wa ukaguzi katika Shirika la Ukaguzi la Tanzania kati ya miaka 1984 na 2000.

Kati ya miaka 2003 na 2009, alifanya kazi kama mhasibu wa Caritas.[1]

Katika siasa

Mabula alijihusisha na CCM mwaka 1990 na kujishughulisha katika majukumu kadha wa kadha ya chama kwenye nyadhifa mbalimbali. Kati ya miaka 2009 na 2015, aliwahi kuwa Kamishna wa Wilaya katika wilaya ya Muleba, Iringa na Butiama kwa mfululizo.[1]

Mabula alichaguliwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015 katika jimbo la Ilemela na kuwashinda wagombea wenzake wanne katika jimbo hilo.[2]

Katika uchaguzi, alikabiliana na mpinzani wake kutoka CHADEMA Highness Kiwia, Mabula alishinda kwa kiasi cha kura 85,424 dhidi ya 61,769.[3]

Katika kipindi cha uchaguzi alipata fedheha kutokana na jinsia yake na hali ya kutokuolewa.[4].

Mabula alichaguliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mazingira na Maendeleo ya Makazi na Jamii katika serikali mpya ya Rais John Magufuli baada ya uchaguzi wa 2015.[5]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 "Profile: Angeline Sylvester Lubala Mabula". Parliament of Tanzania. Iliwekwa mnamo October 16, 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Moses Matthew. "Tanzania: Mwanza Banks on Outgoing MPs for Victory", allAfrica.com, August 5, 2015. 
  3. "CCM regains several seats it lost in 2010", Daily News, October 27, 2015. Retrieved on October 16, 2016. 
  4. Nashon Kennedy. "Fighting gender discrimination, violence to promote gender equality", Daily News, November 12, 2015. Retrieved on October 16, 2016. 
  5. Rose Athumani. "New lean Union cabinet unveiled", Daily News, December 11, 2015. Retrieved on October 16, 2016. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angeline Mabula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.