Frederick Lugard : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Created by translating the page "Frederick Lugard, 1st Baron Lugard"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 08:30, 6 Oktoba 2018

Frederick John Dealtry Lugard (Januari 22, 1858 – Aprili 11, 1945), alikuwa mwanajeshi, mamluki, mpelelezi na mtawala wa koloni. Alikuwa Gavana wa Hong Kong (mwaka 1907-1912), Gavana wa mwisho wa  Nchi Lindwa ya Nijeria Kusini (mwaka 1912-1914), balozi wa kwanza  (mwaka 1900-1906) na gavana wa mwisho (mwaka 1912-1914) wa Nchi Lindwa ya Nijeria Kaskazini na kwanza Gavana Mkuu wa Nijeria (mwaka 1914-1919).

Alizaliwa katika Madras (Chennai), India, lakini alilelewa katika Worcester, Uingereza.[1]

Upelelezi katika Afrika Mashariki

Lugard katika picha iliyochorwa na mwandishi wa jarida la Vanity Fair, mwaka 1895

Baada ya kuondoka Unyasa Aprili, mwaka 1889, Lugard alikubali kufanya kazi katika Kampuni ya Kifalme ya Kiingereza kwa Afrika ya Mashariki (IBEAC). Alifika katika mji wa Mombasa katika Disemba ya mwaka huo. Katika mwaka 1888, IBEAC ilikuwa imepatiwa idhini ya kifalme na Malkia Victoria ili kuangalia uwezo wa kupanua ushawishi katika Zanzibar na Uganda[2] na likuwa na nia ya kufungua njia ya ya biashara kati ya Ziwa Victoria katika Uganda na Bandari ya Mombasa. Kituo cha kwanza cha biashara kilikuwa katika Machakos. Walikuwa wakifika Machakos kupitia njia za zamani ambazo zilikuwa zikipitia Jangwa la Taru, lenye joto kali na vumbi jingi.

Kazi ya kwanza ya Lugard ilikuwa kutafuta njia ya kufikia Machakos ambayo haingepitia Jangwa la Taru.[3] 

Agosti, mwaka 1890, Lugard alisafiri kutoka Mombasa hadi Uganda. Alihakikisha utawala na ushawishi wa Uingereza katika Ufalme wa Buganda na kukomesha ghasia kati ya vikundi tofauti ndani ya ufalme.[4][5]

Alipatiwa jukumu la kufanya makubaliano na makabila wenyeji na kujenga ngome njiani ili kuhakikisha usalama wa ziara ambazo IBEAC ingefanya baadaye.[6] IBEAC ilifanya makubaliano kutumia hati rasmi zilizokuwa zimeandikwa na kutiwa saini na watawala na viongozi wa makabila, lakini Lugard alipendelea kufanya makubaliano ya undugu wa kuchanjiana, kwani aliamini undugu huo uliwasawazisha.[7] Aliingia katika makubaliano kadhaa kama hayo na viongozi wa makabila kati ya Mombasa na Uganda. Mojawapo ya makubaliano ya uchale ambayo ni maarufu yalifanyika mwaka 1890, katika Dagoretti, kati yake na Waiyaki wa Hinga.[8]

Lugard alikuwa mtawala wa jeshi katika Uganda kutoka Disemba 26, mwaka 1890 hadi Mei mwaka 1892. Wakati huo, alizuru Safu ya Ruwenzori hadi Ziwa Edward, akichora ramani ya maeneo hayo. Pia, alisafiri hadi Ziwa Albert na akarudi na maelfu ya Wasudani ambao walikuwa wameachwa na Emin Pasha na H. M. Stanley wakati wa ziara yao.

Huduma katika koloni

Mwaka 1894, Lugard alitumwa na Kampuni ya Kifalme ya Nijeri aende Borgu, ambapo alifanya makubaliano na viongozi ambao walitambua utawala wa Uingereza. Kutoka mwaka 1896 hadi mwaka 1897, Lugard aliongoza msafara wa kuenda katika Ziwa Ngami, Botswana. Baadaye, alitumwa Koloni ya Lagos na bara Nijeria ili aanzishe jeshi la wenyeji ili lilinde maslahi ya Uingereza dhidi ya Ufaransa. 

Baada ya kuhudumu katika Jeshi la Afrika Magharibi, Lugard aliteuliwa kuwa Balozi wa Nchi Lindwa ya Nijeria Kaskazini. Alisoma tangazo liliotangaza kuundwa kwa nchi lindwa katika Januari 1, 1900.[9] 

Lugard alifanywa shujaa wa ukoo bora mwaka 1901 kwa sababu ya huduma yake katika Nijeria.

Angalia pia

  • Moja kwa moja ya utawala
  • Mheshimiwa Richmond Palmer
  • Orodha ya wakuu wa Hong Kong na elimu
  • Frank Lugard Brayne

Marejeo

  1. Sir Frederick John Dealtry Lugard (1858-1945) - Find A Grave Memorial (13 June 2018).
  2. "The Imperial British East Africa Company - IBEAC", Softkenya.com, 2013-01-10. (en-US) 
  3. Miller, Charles (2015). The Lunatic Express. London: Head of Zeus Ltd. 4022. ISBN 9781784972714. 
  4. The London Quarterly and Holborn Review (in English). E.C. Barton. 1894. p. 330. 
  5. Youé, Christopher P. (2006-01-01). Robert Thorne Coryndon: Proconsular Imperialism in Southern and Eastern Africa, 1897-1925 (in English). Wilfrid Laurier Univ. Press. p. 126. ISBN 9780889205482. 
  6. Nicholls, Christine Stephanie (2005). Red Strangers: The White Tribe of Kenya (in English). Timewell Press. p. 10. ISBN 9781857252064. 
  7. Charles., Miller, (2015). The Lunatic Express. Head of Zeus. p. 4015. ISBN 9781784972714. OCLC 968732897. 
  8. Osborne, Myles; Kent, Susan Kingsley (2015-03-24). Africans and Britons in the Age of Empires, 1660-1980 (in English). Routledge. p. 1. ISBN 9781317514817. 
  9. "The Transfer of Nigeria to the Crown" The Times (London). Thursday, 8 February 1900. Issue 36060, p. 7.