Kinyonga (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 18: Mstari 18:
Kwa jumla kuna nyota nne angavu kiasi, nje ya <big>α</big>Cha ni <big>β</big>Cha (mag 2.2), <big>γ</big>Cha (mag 4.1) na <big>δ</big>Cha (mag 5.5).
Kwa jumla kuna nyota nne angavu kiasi, nje ya <big>α</big>Cha ni <big>β</big>Cha (mag 2.2), <big>γ</big>Cha (mag 4.1) na <big>δ</big>Cha (mag 5.5).


==Tanbihi==
==[[Tanbihi]]==
<references/>
<references/>



Pitio la 19:51, 15 Septemba 2018

Nyota za kundinyota Kinyonga (Chamaeleon) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Kinyonga - Chamaeleon

Kinyonga (kwa Kilatini na Kiingereza Chamaeleon) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Mahali pake

Kinyonga iko karibu na ncha ya anga ya kusini. Inapakana na kundinyota Nzi ( Musca), Mkuku (en:Carina) na Panzimaji (en:Volans) upande wa kaskazini, Meza (en:Mensa) upande wa mashariki, Thumni (Octans) upande wa kusini na Ndege wa Peponi (Apus) upande wa magharibi.

Jina

Kinyonga ni kati ya kundinyota zilizobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16. Hazikujulikani kwa Wagiriki wa Kale au Waarabu waliojifunza kutoka kwao. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya Johann Bayer[2].

Keyser alitumia jina la Kiholanzi la Het Chameljoen (Kinyonga) iliyotajwa baadaye kwa jina la Kigirikiki „Chamaeleon“.

Leo iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [3]. Kifupi rasmi ni ‘Cha’.

Nyota

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Chamaeleontis yenye uangavu unaoonekana wa 4.07 mag ikiwa na umbali wa Dunia wa miaka ya nuru 63.5[4]

Kwa jumla kuna nyota nne angavu kiasi, nje ya αCha ni βCha (mag 2.2), γCha (mag 4.1) na δCha (mag 5.5).

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Chamaeleon" katika lugha ya Kilatini ni "Chamaeleontis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Chamaeleontis, nk.
  2. Allen (tazama marejeo) hakuwa na habari za Placius hivyo aliandika ni Bayer aliyetangaza Kinyonga mara ya kwanza.
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Alpha Cha (Alpha Chamaeleontis), tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje