Jamhuri ya Kijamaa ya Kisovyeti ya Kikazakhi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Replacing Flag_of_Kazakh_SSR.svg with File:Flag_of_the_Kazakh_SSR.svg (by CommonsDelinker because: File renamed: standardizin').
Svg version (GlobalReplace v0.6.5)
Mstari 6: Mstari 6:
| [[Picha:COA Kazakh SSR.png|80px|Nembo la Kazakhstan ya Kisovyeti]]
| [[Picha:COA Kazakh SSR.png|80px|Nembo la Kazakhstan ya Kisovyeti]]
|- align=center
|- align=center
| colspan="2" style="background:#ffffff;" | [[Picha:SovietUnionKazakhstan.png|Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti]]<br />''Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti''
| colspan="2" style="background:#ffffff;" | [[Picha:Soviet Union - Kazakh SSR.svg|Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti]]<br />''Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti''
|- align=center
|- align=center
| colspan="2" style="background:#ffffff;" |'''Wito la Umoja wa Kisovyeti: <br />Барлық елдердің
| colspan="2" style="background:#ffffff;" |'''Wito la Umoja wa Kisovyeti: <br />Барлық елдердің

Pitio la 02:35, 12 Septemba 2018

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi
Қазақ Советтік Социалистік Республикасы
Казахская Советская Социалистическая Республика

(Kasak Sovyettik Sotsialistik Respublikasi
Kazakhskaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Respublika)
Bendera ya Kazakhstan ya Kisovyeti Nembo la Kazakhstan ya Kisovyeti
Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti
Jamhuri ya Kikazakhi ndani ya Umoja wa Kisoveti
Wito la Umoja wa Kisovyeti:
Барлық елдердің

пролетарлары, бірігіңдер!
(Kikazakhi: Wafanyakazi wa nchi zote muungane!)

Lugha rasmi hali halisi Kikazakhi na Kirusi
Mji Mkuu Alma-Ata (leo: Almaty)
Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Kazakhstan Nursultan Nasarbajew
Kuanzishwa kama Jamhuri
- Jamhuri ndani ya Umoja wa Kisoveti
- kufutwa
26 Agosti 1920

30 Desemba 1922

16 Desemba 1991
Eneo

- % maji

2,717,300 km²
(wa pili katika Umoja wa Kisovyeti)
1.7%
Wakazi 16,711,900 (sensa 1989)
Msongamano 6.1/km²
Pesa Rubel (рубль)
Kanda za Wakati UTC +4 hadi +6

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi (; Kirusi: Казахская Советская Социалистическая Республика) ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Jina lake liliandikwa kwa Kikirili katika lugha ya Kikazakhi: "Қазақ Советтік Социалистік Республикасы" (Kasak Sovyettik Sotsialistik Respublikasi) au kwa Kirusi: "Казахская Советская Социалистическая Республика" (Kazakhskaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Respublika).

Yenye eneo la 2,717,300 km² ilikuwa jamhuri kubwa ya pili ndani ya Umoja wa Kisovyeti baada ya Urusi. Mji mkuu ulikuwa Alma-Ata inayoitwa leo Almaty. Tangu Desemba 1991 imekuwa nchi huria ya Kazakhstan katika Asia ya Kati.

Historia

Jina la nchi limetokana na Wakazakhi ambao ni taifa la watu wenye lugha ya Kiturki. Eneo liliwahi kuwa sehemu ya milki mbalimbali lakini tangu karne ya 15 Wakazakhi walijaribu kuungana mata kadhaa bila mafanikio ya kudumu. Tangu karne ya 17 milki ya Urusi ilianza kuenea katika Asia ya Kati na hadi 1865 eneo lote la Kazakhstan lilitawaliwa na Urusi.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 Wakomunisti walichukua nafasi ya Matsar wa awali wakafanya nchi kuwa jamhuri yenye kiwango cha kujitawala ndani ya Jamhuri ya Kirusi ya Umoja wa Kisovyeti.

1936 nchi ilipewa cheo cha jamhuri kamili ya Umoja wa Kisovyeti. Katika miaka iliyofuata Warusi na watu wa mataifa mengine ya Umoja walihamishwa nchini hadi Wakazakhi kuwa chini ya nusu ya wakazi wote.

1990/1991 wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti jamhuri ilijiondoa polepole. Kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Kazakhstan Nursultan Nasarbajew alitangaza uhuru na kuwa rais wa kwanza akiendelea kutawala jinsi awali.

Uchumi

Wakomunisti walifanya jitihadi kubwa kuchimba madini na kuanzisha viwanda pamoja na kupanusha kilimo. Miradi mikubwa ya kumwagilia ardhi yabisi yaliwezesha mavuno makubwa lakini yalisababisha pia kukauka kwa ziwa Aral.

Umoja wa Kisovyeti ilijenga uwanja wa roketi wa Baikonur uliokuwa kituo kikuu cha kurusha vyombo vya angani.