Kaizari : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaisari --> Kaizari
d Kaisari moved to Kaizari over redirect: Maandishi rasmi kulingana na kamusi ya TUKI (matamshi ya Kijerumani ''Kaiser'' pia ni kwa kutamka ''z'').
(Hakuna tofauti)

Pitio la 18:43, 6 Januari 2008

Julius Caesar alikuwa asili ya cheo cha Kaizari
Kaizari Augusto wa Dola la Roma
Mtawala wa Ufaransa Napoleon Bonaparte aliyejiwekea taji la Kaizari 1804
Kaizari Bokassa 1977

Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani.

Asili ya Kiroma

Asili yake ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina lilikuwa cheo.

Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki (Bizanti) hadi 1453.

Ulaya

Katika Ulaya yenyewe mfalme wa Wafranki Karolo Mkuu alipokea cheo cha "Caesar" au Kaizari. Baadaye wafalme Wajerumani waliomfuata Karolo Mkuu katika sehemu ya mashariki ya ufalme wake waliendelea kutumia cheo hiki cha Caesar au Kaizari.

Neno la Kaizari liliingia katika lugha ya Kiswahili wakati wa ukoloni wa Kijerumani huko Tanzania. Austria na Ujerumani zilitawaliwa hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia 1918 na wafalme wenye cheo cha "Kaizari" (kijer.: Kaiser).

Vilevile mfalme wa Urusi alikuwa na cheo kilekile kilichoitwa "Tsar" kwa Kirusi, ilhali neno hili limeundwa pia kutoka kwa "Caesar".

Lugha za Kiingerezea na Kifaransa zilitumia cheo tofauti cha macaesar wa Kiroma ndicho "Imperator" (=mwenye amri, mwenye mamlaka, jemadari) kilichokuwa "Emperor" (Kiing.) au "Empereur" (Kifaransa).

Nje ya Ulaya

Kaizari ni cheo cha mfalme aliye juu ya wafalme wengine. Kutokana na uzuefu huu hata Shah wa Uajemi, Tenno wa Japani, Huangdi wa China na Negus Negesti wa Ethiopia hutajwa kwa cheo cha "Kaizari".

Malkia Viktoria alitumia cheo cha Kaizari ("empress") kama mtawala wa Uhindi tangu 1877.

Rais Jean-Bedel Bokassa alijitangaza kuwa Kaizari ("empereur") wa Afrika ya Kati mwaka 1977 akiiga mfano wa Napoleon Bonaparte aliyejiwekea taji la Kaizari ya Ufaransa mwaka 1804. Bokassa alipinduliwa 1979 na nchi kuwa jamhuri tena.