Galaksi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
masahihisho madogo
masahihisho madogo
Mstari 5: Mstari 5:
Kuna galaksi nyingi sana [[ulimwengu]]ni. Kwa [[wastani]] kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama [[bilioni]] 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.
Kuna galaksi nyingi sana [[ulimwengu]]ni. Kwa [[wastani]] kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama [[bilioni]] 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.


Galaksi yetu, ikiwemo [[mfumo wa jua|mfumo wetu wa jua]], imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama [[kanda]] la kung'aa kwenye [[anga]] la [[usiku]] linalojulikana kwa [[rangi]] yake kama [[njia nyeupe]] au "njia ya [[maziwa]]"<ref>Maziwa (mfano maziwa ya ng'ombe) kwa [[Kigiriki]] huitwa "galaks" na hapo aili ya jina "galaksi".</ref>. Umbo lake unafanana na kisahani kikiwa na [[kipenyo]] cha [[mwaka wa nuru|miaka ya nuru]] 100,000 na kikiwa na [[unene]] wa miaka ya nuru 3,000.
Galaksi yetu, ikiwemo [[mfumo wa jua|mfumo wetu wa jua]], imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama [[kanda]] la kung'aa kwenye [[anga]] la [[usiku]] linalojulikana kwa [[rangi]] yake kama [[njia nyeupe]] au "njia ya [[maziwa]]"<ref>Maziwa (mfano maziwa ya ng'ombe) kwa [[Kigiriki]] huitwa "galaks" na hapo aili ya jina "galaksi".</ref>. Umbo lake linafanana na kisahani kikiwa na [[kipenyo]] cha [[mwaka wa nuru|miaka ya nuru]] 100,000 na kikiwa na [[unene]] wa miaka ya nuru 3,000.


Galaksi iliyo karibu angani inaitwa [[Andromeda (galaksi)|Andromeda]] na ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5.
Galaksi iliyo karibu angani inaitwa [[Andromeda (galaksi)|Andromeda]] na ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5.

Pitio la 20:14, 5 Julai 2018

Galaksi ya Andromeda yenye na. M 31 na galaksi mbili ndogo za kando M 32 na M 110

Galaksi (ing. galaxy) ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga la ulimwengu kutokana na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana.

Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.

Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wetu wa jua, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kwa rangi yake kama njia nyeupe au "njia ya maziwa"[1]. Umbo lake linafanana na kisahani kikiwa na kipenyo cha miaka ya nuru 100,000 na kikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000.

Galaksi iliyo karibu angani inaitwa Andromeda na ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5.

Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi zinazoweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana ni mabilioni. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.

Galaksi zinazojulikana zimepewa namba katika orodha ya kimataifa na wanasayansi wa astronomia.

Galaksi kati yao hujumuika pia zikiathiriana kwa njia ya graviti yao na kuzunguka kitovu cha graviti cha pamoja. Galaksi hadi 50 zinazoshikamana katika kipenyo cha miaka ya nuru milioni 10 huitwa kundi la galaksi (ing. galaxy group). Kuna pia galaksi mamia hadi maelfu kadhaa zinazoshikamana na hii huitwa fundo la galaksi (ing. galaxy cluster) linaweze kuwa na kipenyo ch miaka ya nuru milioni 10 - 20.

Marejeo

  1. Maziwa (mfano maziwa ya ng'ombe) kwa Kigiriki huitwa "galaks" na hapo aili ya jina "galaksi".