Tanzania : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 52: Mstari 52:
'''Tanzania''' ni [[nchi]] iliyoko [[Afrika ya Mashariki]].
'''Tanzania''' ni [[nchi]] iliyoko [[Afrika ya Mashariki]].


Imepakana na [[Uganda]] na [[Kenya]] upande wa [[kaskazini]], [[Bahari Hindi]] upande wa [[mashariki]], [[Msumbiji]], [[Malawi]] na [[Zambia]] upande wa [[kusini]], [[Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia|Kongo]], [[Burundi]] na [[Rwanda]] upande wa [[magharibi]].
Imepakana na [[Uganda]] na [[Kenya]] upande wa [[kaskazini]], [[Bahari Hindi]] upande wa [[mashariki]], [[Msumbiji]], [[Malawi]] na [[Zambia]] upande wa [[kusini]], [[Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia|Kongo]], [[Burundi]] na [[Rwanda]] upande wa [[magharibi]]. Eneo lina [[kilometa za mraba]] 947,303 (nchi ya 31 [[duniani]]); [[maji ya ndani]] yanachukua [[asilimia]] 6.2. Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka [[2012]] walikuwa 44,928,923 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika [[sensa]] ya mwaka [[2002]]. [[Msongamano]] ni wa watu 47.5 kwa [[km2]] (nchi ya 124 duniani). Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa [[Jumuiya ya Afrika ya Mashariki]]. [[Mji mkuu]] ni [[Dodoma mjini|Dodoma]] (wenye wakazi 410,956), lakini [[rais]] bado yupo [[Dar es Salaam]], [[jiji]] kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni 4,364,541. Miji mingine ni kama vile [[Mwanza (mji)|Mwanza]] (706,543), [[Arusha (mji)|Arusha]] (416,442), [[Mbeya (mji)|Mbeya]] (385,279), [[Morogoro (mji)|Morogoro]] (315,866), [[Tanga (mji)|Tanga]] (273,332), [[Kahama (mji)|Kahama]] (242,208), [[Tabora (mji)|Tabora]] (226,999) na [[Zanzibar (Jiji)|Zanzibar]] (223,033).

Eneo lina [[kilometa za mraba]] 947,303 (nchi ya 31 [[duniani]]); [[maji ya ndani]] yanachukua [[asilimia]] 6.2.

Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka [[2012]] walikuwa 44,928,923 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika [[sensa]] ya mwaka [[2002]].

[[Msongamano]] ni wa watu 47.5 kwa [[km2]] (nchi ya 124 duniani).

Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa [[Jumuiya ya Afrika ya Mashariki]].

[[Mji mkuu]] ni [[Dodoma mjini|Dodoma]] (wenye wakazi 410,956), lakini [[rais]] bado yupo [[Dar es Salaam]], [[jiji]] kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni 4,364,541.

Miji mingine ni kama vile [[Mwanza (mji)|Mwanza]] (706,543), [[Arusha (mji)|Arusha]] (416,442), [[Mbeya (mji)|Mbeya]] (385,279), [[Morogoro (mji)|Morogoro]] (315,866), [[Tanga (mji)|Tanga]] (273,332), [[Kahama (mji)|Kahama]] (242,208), [[Tabora (mji)|Tabora]] (226,999) na [[Zanzibar (Jiji)|Zanzibar]] (223,033).


==Jiografia==
==Jiografia==
Nchi iko katika eneo la [[Maziwa makubwa ya Afrika]], hivyo [[Ziwa|maziwa]] yanafunika km<sup>2</sup> 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi. Pia ina [[mito]] mingi ambayo inaelekeza [[maji]] yake katika [[Bahari ya Hindi]] [[mashariki]] mwa nchi, lakini mingine inachangia [[Mto Zambezi]] kupitia [[Ziwa Nyasa]], michache [[Bahari ya Kati]] kupitia [[Ziwa Victoria]] na [[mto Naili]], mingine tena [[Bahari Atlantiki]] kupitia [[Ziwa Tanganyika]] na mingine inaishia katika [[mabonde]] kama ya [[Ziwa Rukwa]]. Karibu [[thuluthi]] [[moja]] ya nchi inalindwa kwa namna moja au nyingine: kuna [[Mbuga za Taifa la Tanzania|Hifadhi za Taifa 16]], mbali ya Hifadhi Teule, Hifadhi za Mawindo, Mapori ya Akiba n.k.
Nchi iko katika eneo la [[Maziwa makubwa ya Afrika]], hivyo [[Ziwa|maziwa]] yanafunika km<sup>2</sup> 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi.

Pia ina [[mito]] mingi ambayo inaelekeza [[maji]] yake katika [[Bahari ya Hindi]] [[mashariki]] mwa nchi, lakini mingine inachangia [[Mto Zambezi]] kupitia [[Ziwa Nyasa]], michache [[Bahari ya Kati]] kupitia [[Ziwa Victoria]] na [[mto Naili]], mingine tena [[Bahari Atlantiki]] kupitia [[Ziwa Tanganyika]] na mingine inaishia katika [[mabonde]] kama ya [[Ziwa Rukwa]].

Karibu [[thuluthi]] [[moja]] ya nchi inalindwa kwa namna moja au nyingine: kuna [[Mbuga za Taifa la Tanzania|Hifadhi za Taifa 16]], mbali ya Hifadhi Teule, Hifadhi za Mawindo, Mapori ya Akiba n.k.


== Historia ==
== Historia ==

Pitio la 18:32, 17 Juni 2018

The United Republic of Tanzania (Kiing.)
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
(Kiswahili)
Bendera ya Tanzania Nembo ya Tanzania
Bendera ya Tanzania Nembo ya Tanzania

Kaulimbiu: Uhuru na Umoja

Wimbo wa Taifa Mungu ibariki Afrika
Lugha rasmi Kiswahili (kwa dhati)
Mji Mkuu Dodoma
Makao ya Serikali Dodoma
Serikali Jamhuri
Rais John Pombe Joseph Magufuli
Makamu wa Rais Samia Suluhu
Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa
Eneo km² 947.303
Wakazi 51,820,000 [2] (28th) (2014)
Wakazi kwa km² 47.5
Uhuru Tanganyika kutoka Uingereza 9 Desemba 1961; mapinduzi Zanzibar 12 Januari 1964; muungano Tanganyika na Zanzibar 26 Aprili 1964
Pesa Shilingi ya Tanzania
Wakati UTC+3
Dini za wakazi Dini asilia za Kiafrika (34.3%), Ukristo (33.5%), Uislamu (31.4%), wengineo (0.8%){{Sensa ya 27 Agosti 1967[1]}}
Tanzania katika Afrika
Ramani ya mikoa ya Tanzania tangu mwaka 2012

Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki.

Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi. Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 walikuwa 44,928,923 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2002. Msongamano ni wa watu 47.5 kwa km2 (nchi ya 124 duniani). Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 410,956), lakini rais bado yupo Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni 4,364,541. Miji mingine ni kama vile Mwanza (706,543), Arusha (416,442), Mbeya (385,279), Morogoro (315,866), Tanga (273,332), Kahama (242,208), Tabora (226,999) na Zanzibar (223,033).

Jiografia

Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa yanafunika km2 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi. Pia ina mito mingi ambayo inaelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi, lakini mingine inachangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, michache Bahari ya Kati kupitia Ziwa Victoria na mto Naili, mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika na mingine inaishia katika mabonde kama ya Ziwa Rukwa. Karibu thuluthi moja ya nchi inalindwa kwa namna moja au nyingine: kuna Hifadhi za Taifa 16, mbali ya Hifadhi Teule, Hifadhi za Mawindo, Mapori ya Akiba n.k.

Historia

(Kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)

Jina "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar (pamoja na athira ya jina la kale la "AzanIA").

Nchi hizo mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa makoloni ya kawaida.

Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza).

Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa lililoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.

Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995-2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa.

Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005-2015), naye aliendeleza sera za watangulizi wake akitokea chama hichohicho cha CCM.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa rais wa awamu ya tano, John Magufuli (wa CCM vilevile).

Miundo ya muungano

Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar kufanyika mwaka 1964 Tanzania imekuwa na miundo ifuatayo:

Mambo yafuatayo yamekubalika kuwa shughuli za muungano:

  • Mambo ya nje
  • Jeshi
  • Polisi
  • Mamlaka ya dharura
  • Uraia
  • Uhamiaji
  • Biashara ya nje
  • Utumishi wa umma
  • Kodi ya mapato, forodha
  • Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu

Utawala

Muundo wa uongozi na utawala katika kipindi cha ukoloni ulizingatia mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya dola yaani utawala, bunge na mahakama.

Mgawanyo huu umeainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 4(1).

Tangu uhuru, mgawanyo wa madaraka na uhusiano miongoni mwa mihimili hiyo uliimarishwa ipasavyo kwa kuzingatia wakati, mahitaji ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Mgawanyo wa kiutawala wa Tanzania unafuata Katiba ya nchi I 2.2. Tanzania imegawiwa kwa mikoa 31. Kila mkoa huwa na wilaya ndani yake. Jumla ya wilaya ni 169, ambazo kati yake 34 ni miji.

Ndani ya wilaya kuna ngazi za tarafa (division) na kata (ward).

Chini ya kata kuna vijiji na wakati mwingine ngazi ya chini tena ambayo ni vitongoji.

Mkoa Makao Makuu Mkoa Makao Makuu
Arusha Arusha Mwanza Mwanza
Dar es Salaam Dar es Salaam Njombe Njombe
Dodoma Dodoma Pemba Kaskazini Wete
Geita Geita Pemba Kusini Chake Chake
Iringa Iringa Pwani Kibaha
Kagera Bukoba Rukwa Sumbawanga
Katavi Mpanda Ruvuma Songea
Kigoma Kigoma Shinyanga Shinyanga
Kilimanjaro Moshi Simiyu Bariadi
Lindi Lindi Singida Singida
Manyara Babati Tabora Tabora
Mara Musoma Tanga Tanga
Mbeya Mbeya Zanzibar Kati/Kusini Koani
Morogoro Morogoro Unguja Kaskazini Mkokotoni
Mtwara Mtwara Unguja Magharibi Zanzibar

Watu

Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kwa wastani kuna mtu mmoja tu kwa kilomita ya mraba (1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba na katika Mkoa wa Dar es Salaam ni 3,133 kwa kilomita ya mraba.

Asilimia 70 hivi huishi vijijini.

Makabila

Jamii nyingi za watu zimeishi na kushirikiana katika eneo la Tanzania bara kwa milenia nyingi.

Kati ya jamii hizo, nyingi zilikuja kutoka maeneo mengine ya Afrika.

Nyingi katika jamii zilizohamia sehemu hii ziliingia katika makundi madogomadogo kwa amani, ingawa ziko zilizoingia kwa njia ya uvamizi na vita. Baadhi ya jamii zilizovamiwa zilijihami na kuwazuia wahamiaji wasiendelee kuteka maeneo mengine.

Kufikia mwaka 1884, wakati Wajerumani walipoanza harakati za kufanya sehemu hii ya Afrika kuwa koloni lao, kulikuwa na makabila zaidi ya 120 katika eneo la Tanzania bara.

Kuna makabila 125 hivi. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya, Wajaluo na Wamakonde.

Jambo la pekee kuhusu jamii zilizoishi na zinazoendelea kuishi Tanzania ni kwamba wakazi asili wanawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika[2].

1. Idadi kubwa sana ya Watanzania ni wa jamii ya Wabantu (k.m. Wazaramo, Wagogo, Wasukuma, Wahaya, Wachaga, Wapare na Wapogoro).

2. Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya.

3. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome na Wasi.

4. Kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina yao ni Wasandawe na Waburunge.

Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati.

Pia kuna asilimia ndogo ya watu wenye asili ya nje ya bara la Afrika, kwa mfano Wahindi, Waarabu, Waindochina, Wafarsi, Wachina na Waingereza. Hii ilisababishwa na karne za mchanganyiko wa mahitaji ya biashara yaliyofanywa na mabara ya Ulaya na Asia hapo Afrika.

Lugha

Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya mia moja na ishirini, kwa kuwa kila kabila lina lugha yake.

Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na inazidi kuwa lugha mama kwa watoto wengi, hasa mijini[3]. Walau asilimia 90 za wakazi wanakitumia walau kama lugha ya pili. Kiswahili ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu: hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini, kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu. Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo rasmi; kwa hiyo ni lugha rasmi ya dhati.

Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari ingawa sera mpya inataka Kiswahili kishike nafasi yake hadi chuo kikuu[4]; kwa hiyo ilichukuliwa kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi rasmi wa Kiingereza umepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati pekee.

Sera mpya ya elimu inakusudia kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote kufikia mwaka 2024.

Dini

Kanisa kuu la Arusha

Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi inawezekana ni zaidi azimio la kisiasa.

Kwenye visiwa vya Zanzibar idadi ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 97%.

Usafiri

Usafiri wa Tanzania: Kusukuma basi wakati wa mvua kwenye barabara ya kwenda Mbamba Bay (mwaka 2012)

Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Nyingine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani ya Bahari Hindi kuna pia usafiri wa meli.

Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-magharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu.

Mashirika mawili ya reli yanayohudumia Tanzania: ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali.

Huduma kwa ndege zatumia hasa viwanja vya ndege 11 vyenye barabara ya lami kwa ajili ya ndege, hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni. Pia kuna viwanja vingine vya ndege ambavyo ni uwanja wa ndege wa Mwanza, Bukoba na Kigoma.

Usafiri wa majini pia unafanyika hasa katika bahari ya Hindi, hakuna meli ya serikali hapo na mashirika binafsi hutoa huduma. Usafiri wa majini hufanyika pia katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa. Miongoni mwa Meli ni MV Bukoba iliyozama mwaka 1996

Katika ziwa Tanganyika ipo meli ya Mv Liemba ambayo ilianza kutumika tangia kipindi cha ukoloni was wajerumani, inatoa huduma kati ya miji ya mwambao wa ziwa Tanganyika na nchi jirani

Mwaka 2017 ulianza ujenzi wa awamu ya kwanza ya njia ya geji sanifu nchini Tanzania inayolenga kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro[5]. Njia hii inatarajiwa kuendelea hadi Mwanza na hatimaye hadi Burundi.

Utamaduni na sanaa

Bombwe la Kimakonde: Tembo

Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.

Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.

Tangu miaka ya 1970 uchoraji wa "tingatinga" umejulikana: ulipata jina hilo kutoka kwa Edward Tingatinga naye mtu wa Umakonde.

Utamaduni wa Watanzania ni pamoja na utaraab. Muziki ana nyimbo za kitaraab ndizo muhimu sana kwa nchi nzima, hasa visiwani na pwani. Pia kuna miziki ya Kinyarwanda, dansi kama intore n.k.

Urithi wa Dunia

Mchoro wa mwaka 1572 ukionyesha mji wa Kilwa ulivyokuwa wakati huo.

Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)

Tazama pia

Tanbihi

  1. International Religious Freedom Report 2007: Tanzania. United States Bureau of Democracy, Human Rights and Labor (14 Septemba 2007). This article incorporates text from this source, which is in the public domain.
  2. Ulrich Ammon; Norbert Dittmar; Klaus J. Mattheier (2006). Sociolinguistics: An International Handbook of the Science of Language and Society. Walter de Gruyter. pp. 1967–. ISBN 978-3-11-018418-1.
  3. Concise Encyclopedia of Languages of the World. Elsevier. 2010. pp. 1026–. ISBN 978-0-08-087775-4.
  4. "Tanzania Ditches English In Education Overhaul Plan". AFK Insider. 17 February 2015. Retrieved 23 February 2015.
  5. Turkish, Portuguese firms win bid to construct Tanzania’s SGR, tovuti ya theeastafrican.co.ke ya 6 Februari 2017, iliangaliwa Mei 2017

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:



Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tanzania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.