Pangani (mto) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 13: Mstari 13:


==Beseni la mto==
==Beseni la mto==
[[Picha:Pangani_River2.jpg|right|thumb|Mto Pangani kwenye [[Pangani mjini]]]]
[[Beseni]] la Pangani ni eneo la km<sup>2</sup> 43,650. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna km<sup>2</sup> 3,914 huko [[Kenya]] katika [[mazingira]] ya [[Taveta]]. Jumla ya wakazi katika beseni la Pangani ni [[milioni]] 3.7.
[[Beseni]] la Pangani ni eneo la km<sup>2</sup> 43,650. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna km<sup>2</sup> 3,914 huko [[Kenya]] katika [[mazingira]] ya [[Taveta]]. Jumla ya wakazi katika beseni la Pangani ni [[milioni]] 3.7.



Pitio la 15:11, 27 Mei 2018

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia hapa Pangani

Beseni ya Mto Pangani.

Mto Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani.

Jina

Mto unapita katika maeneo ya jumuiya zenye lugha tofautitofauti, hivyo kuna majina mbalimbali.

Katika karne ya 19 kabla ya ukoloni mwendo hadi maporomoko karibu na Hale (Mnyuzi) ulijulikana zaidi kama "Ruvu", na sehemu ya mwisho kuanzia maporomoko hadi bahari kwa jina "Pangani" kutokana na mji ulipofikia baharini[1] .

Kwenye ramani za zamani za ukoloni majina yote mawili yalitumika kandokando: "Ruvu" na "Pangani". Ramani za zamani za uhuru wa Tanzania mara nyingi huwa na maandishi "Pangani or Ruvu River". [2].

Siku hizi imekuwa kawaida kutumia jina "Pangani" kuanzia bwawa la Nyumba ya Mungu.

Beseni la mto

Mto Pangani kwenye Pangani mjini

Beseni la Pangani ni eneo la km2 43,650. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna km2 3,914 huko Kenya katika mazingira ya Taveta. Jumla ya wakazi katika beseni la Pangani ni milioni 3.7.

Chanzo cha mto Pangani ni maungano ya tawimito Kikuletwa na Ruvu inayokutana leo katika lambo la Nyumba ya Mungu kusini kwa Moshi. Mto Kikuletwa hupokea maji kutoka Mlima Meru na mitelemko ya Kilimanjaro upande wa kusini. Ruvu hupokea maji kutoka mitelemko ya Kilimanjaro upande wa mashariki pamoja na Ziwa la Jipe.

Mto Pangani unaendelea km 432 hadi Pangani mjini unapoingia katika Bahari Hindi. Kwenye sehemu ya kwanza baada ya Nyumba ya Mungu mto unaitwa wakati mwingine bado "Ruvu".

Uzalishaji wa umeme kwenye mto Pangani

Kituo cha umeme mtoni Pangani

Kuna mahali pawili ambako malambo yametengenezwa kutumia umememaji ya mto Pangani

Vituo vya umeme vimeathiriwa vibaya na kupungukiwa kwa maji mtoni.[3]

Hifadhi ya mazingira na kupungukiwa kwa maji

Mto Pangani unategemea misitu panapokusanywa maji yake. Misitu hii imepungua sana kutokana na uenezaji wa mashamba, kukatwa kwa miti kwa ajili ya makaa na matumizi ya ubao[4].

Vilevile machafuko yamekuwa hatari kwa ajili ya afya ya mto na watu wanaotegemea maji yake. Asili ya machafuko ni hasa kilimo, mvua hupeleka mbolea mtoni na kusababisha kukua kwa wingi wa majani yasiyotakika.

Uvuvi umezidi vilevile hadi kuhatarisha samaki.

Marejeo

  1. Royal Geographical Society (Great Britain); Shaw, Norton; Galton, Sir Francis; Sir Clements Robert Markham, William Spottiswoode, Henry Walter Bates, Sir John Scott Keltie (1875). Proceedings ... (toleo la Now in the public domain.). ku. 318–. Iliwekwa mnamo 9 October 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. cf the map Sheet SB 37/2, Series Y401, by War Office 1946 of 1946 and this map from 1960 Sheet SB-37-2 Series Y503, Edition 1-TSD, Published by the Survey Division, Ministry of Lands, Survey and Water, Tanganyika 1960, both showing "Pangani or Ruvu River" as name
  3. Evaluation of the Suitability of Pangan i Falls Redevelopment (Hydro Power) Project in Pangani River Basin, Tanzania: An IWRM Approach, by Kimwaga, R.J. and Nkandi, S., tovuti ya Chuo kikuu cha Giessen, Ujeruamni, ilitazamiwa Mei 2016
  4. Water Security in Pangani, taarifa juu ya kukauka kwa mto Ruvu na bwawa la Nyumba ya Mungu, tovuti ya SIU-Norwei ya 2008, ilitazamiwa Mei 2016

Viungo vya nje