Kisukuku : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
masahihisho ya lugha
Mstari 29: Mstari 29:


==Tazama pia==
==Tazama pia==
*[[Fueli za kisikuku]]
*[[Fueli za kisukuku]]


{{mbegu-sayansi}}
{{mbegu-sayansi}}

Pitio la 05:58, 18 Mei 2018

Kiunzi cha mifupa cha Ichthyosauria (sauri ya bahari) kilichopatikana Ujerumani kusini aliyeishi takriban miaka milioni 200 - 100 iliyopita
Trilobiti walikuwa viumbe vya miaka milioni 444 iliyopita.
Mti uliokuwa jiwe
Archeopteryx ni ndege wa kwanza anayejulikana kutokana na visukuku akifanana bado na reptilia lakini anaonyesha manyoa tayari

Kisukuku (ing. fossile) ni mabaki ya viumbehai au mimea au wanyama kutoka zamani za miaka 10,000 au zaidi. Visukuku vingi vina umri wa miaka mamilioni.

Mabaki yanapatikana kwa umbo tofautitofauti, hasa kama

  • visukuku vya kijiwe vinavyoweza kutupa picha ya viumbehai vya nyakati zilizopita, na
  • visukuku vya makaa na mafuta ambavyo ni chanzo muhimu cha nishati

Visukuku vya kijiwe

Mara nyingi miili ya wanyama na mimea imehifadhiwa kwa umbo la jiwe. Ni kama picha au au hata sanamu ya kiumbe kile. Mifano bora imepatikana pale ambako mmea au mwili wa mnyama ulianguka katika matope laini na kuzama chini haraka. Ndani ya matope laini mwili haukuoza shauri la uhaba wa oksijeni na uhaba wa bakteria. Polepole maji ya matope yaliingia dani ya mwili na kujaza nafasi zilizojazwa awali na kiowevu cha seli wakati kiumbe kilikuwa hai. Maji ya matope yalipeleka pia minerali mbalimbali ndani ya mwili. Jinsi mwendo huu uliweza kuendelea bila kuzuiliwa polepole hata seli ziliweza kujazwa kwa vipande vidogo vya matope na minerali nyingine. Kama baada ya miaka mingi matope yalikauka hata matope ndani ya seli za mwili ulikauka lakini kwa kutunza umbo la seli hizi. Kama ganda la matope liliendelea kufunikwa na tabaka za udongo wa juu shindikizo la juu lilianza kubadilisha ule udongo kuwa jiwe na mwamba kabisa.

Kama mwili mwenyewe umeshaoza hadi kiunzi cha mifupa kilifunikwa kuna pia visukuku vya mifupa tu. Viumbe kama konokono mara nyingi viliacha visukuku vya umbo la nje pekee kwa sababu miili yao ni laini sana ilipotea haraka na ganda lao halikubali maji yenye mineral kuingia ndani yake.

Sehemu ambako mazingira yalifaa kwa kutokea kwa visukuku huitwa "Lagerstätte" na wataalamu (la-ger-ste-te, neno la kijerumani) na hapa mifano mingi imewahi kuchimbwa. Kutokana na mwendo wa gandunia (yaani kukunjwa kwa ganda la Dunia) sehemu hizi zinaweza kupatikana chini ya ardhi au juu mlimani.

Kwa njia hii ilitokea mifano kamili ya miili ya spishi zisizopatikana tena duniani. Wataalamu hulinganisha visukuku na wanyama au mimea ya leo na hap wanapata picha juu ya mabadiliko ya spishi. Nadharia ya mageuko ya spishi iliathiriwa sana na matokeo ya utafiti wa visukuku.

Aina ya pekee ya visukuku ni wadudu waliofungwa ndani ya utomvi wa miti uliobadilika baadaye kuwa kaharabu.

Visikuku vya makaa na mafuta

Sehemu kubwa ya mimea ya kale haikugeukiwa kuwa visikuku vya kijiwe bali mabaki yao yalibadilika wakati yalipokaa kama tabaka juu ya uso wa ardhi yalifunikwa kwa udongo na kubadilishwa kwa shindikizo na joto.

Makaa yote yaliyopo chini ya ardhi ni matokeo ya m chakato huu; ndani ya makaa wakati mwingine sehemu za miti bado zinaonekana lakini zimebadilishwa kuwa makaa. Hivyo asili ya makaa ni hasa misitu ya kale na miti yao.

Mafuta ya petroli imetokana na algae na mimea mingine ya baharini. Baada ya kufa mabaki yao yalizama chini hadi sakafu ya bahari. Kutokana na uhaba wa oksijeni hapo chini mabaki hayakuoza na tabaka nene za matope zilitokea. Kama maganda haya yalifunkiwa polepole na udongo na minerali nyingine kulitokea mchakato wa mabadiliko kutokana na shindikizo na joto. Mchakato huu ulibadilisha matope ya mimea kuwa mafuta ya petroli. Hapa ilitokea pia gesi. Pale ambako gesi hii ilifungwa chini ya takaba ya miamba isiyopitika tunakuta siku hizi akiba za gesi asilia zinazofikiwa kwa kutoboa miamba na kupeleka gesi kwa mabomba pale inapotumiwa.

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisukuku kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.