Kishawishi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 14 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q1053973 (translate me)
Mstari 9: Mstari 9:
==Yesu==
==Yesu==
[[Injili]] zinasimulia pia vishawishi vilivyompata [[Yesu]], hasa vitatu vilivyosababishwa na shetani [[jangwa]]ni, ambavyo Yesu alivishinda moja kwa moja na hivyo kutuelekeza namna ya kuvishinda vilevile.
[[Injili]] zinasimulia pia vishawishi vilivyompata [[Yesu]], hasa vitatu vilivyosababishwa na shetani [[jangwa]]ni, ambavyo Yesu alivishinda moja kwa moja na hivyo kutuelekeza namna ya kuvishinda vilevile.

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, “hata mauti, naam, mauti ya msalaba” ([[Fil]] 2:8). “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” ([[Rom]] 5:19).


==Baba Yetu==
==Baba Yetu==

Pitio la 10:54, 5 Aprili 2018

Adamu na Eva wakishawishiwa katika bustani.

Kishawishi ni tendo la kumvuta binadamu kutenda jambo. Mara nyingi maana yake ni mbaya, yaani ni kumvuta atende dhambi.

Kishawishi kinaweza kujianzia au kutokana na watu wengine, lakini dini, kama vile Ukristo, zinaweza kuona nyuma yake hasa uwepo wa nguvu za giza, hususan shetani au ibilisi.

Adamu na Eva

Katika Biblia kishawishi cha kwanza kiliwapata na kuwashinda Adamu na mke wake Eva. Tukio hilo maarufu kwa jina la dhambi ya asili limeathiri binadamu wote.

Yesu

Injili zinasimulia pia vishawishi vilivyompata Yesu, hasa vitatu vilivyosababishwa na shetani jangwani, ambavyo Yesu alivishinda moja kwa moja na hivyo kutuelekeza namna ya kuvishinda vilevile.

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, “hata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8). “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rom 5:19).

Baba Yetu

Sala ya Baba Yetu ambayo Yesi aliwafundisha mitume wake inamalizika kwa kuomba ushindi dhidi ya vishavishi na ya Yule Mwovu (Math 6:13).