Isilandi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
update
Mstari 77: Mstari 77:


== Historia ==
== Historia ==
=== Historia ya awali===
Iceland iko mbali na [[bara]] la [[Ulaya]] na la [[Amerika]] tena katika [[mazingira]] ya [[baridi]]. Inaaminika haikuwa na watu kabisa hadi mwaka [[800]] [[BK]]. [[Wataalamu]] hawakubaliani kama ni ma[[baharia]] kutoka [[Norwei]] au [[Ueire]] waliobahatika kufika kisiwani na kujenga makao ya kwanza.
Iceland iko mbali na [[bara]] la [[Ulaya]] na la [[Amerika]] tena katika [[mazingira]] ya [[baridi]]. Hivyo inaaminika haikuwa na [[watu]] kabisa hadi mwaka [[800]] [[BK]]. [[Wataalamu]] hawakubaliani kama ni ma[[baharia]] kutoka [[Norwei]] au [[Eire]] waliobahatika kufika [[Kisiwa|kisiwani]] na kujenga makao ya kwanza.


Hakika waliofika wengi kidogo walikuwa [[Waviking]] au Wa[[norwei]] wa kale katika [[karne ya 9]]. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwa jina alikuwa [[Flóki Vilgerðarson]].
Hakika waliofika wengi kidogo walikuwa [[Waviking]] au Wa[[norwei]] wa kale katika [[karne ya 9]]. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwa [[jina]] alikuwa [[Flóki Vilgerðarson]].


Waviking waliofika walikuja pamoja na [[familia]] na [[watumishi]] au [[watumwa]] wao. Mnamo mwaka [[930]] ma[[chifu]] na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina ya [[katiba]] kwa Iceland. Walianzisha [[bunge]] la [[Althing]]. Ulikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa na cheo cha kuunganisha madaraka ya [[chifu]], [[hakimu]] na [[kuhani]]. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Iceland ni nchi ya pekee ambako utaratibu wa ki[[demokrasia]] wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi ya wafalme au watawala wengine iliongezeka na kumeza [[haki]] zote za watu wa kawaida.
Waviking waliofika walikuja pamoja na [[familia]] na [[watumishi]] au [[watumwa]] wao. Mnamo mwaka [[930]] ma[[chifu]] na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina ya [[katiba]] kwa Iceland. Walianzisha [[bunge]] la [[Althing]]. Ulikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa na [[cheo]] cha kuunganisha [[madaraka]] ya [[chifu]], [[hakimu]] na [[kuhani]]. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Iceland ni nchi ya pekee ambako utaratibu wa ki[[demokrasia]] wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi ya [[wafalme]] au [[watawala]] wengine iliongezeka na kumeza [[haki]] zote za watu wa kawaida.


Mwaka [[985]] Mwiceland aligundua njia ya kufika [[Greenland]] na baadaye [[Amerika ya Kaskazini]]. Mviking mmoja kwa jina "[[Erik Mwekundu]]" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwa [[mwuaji]]. Alielekea magharibi kwa [[jahazi]] yake na kufika kwanza Greenland halafu [[pwani]] ya [[Kanada]] ya leo. Aliita bara jipya "nchi ya [[mzabibu]]" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila ma[[tunda]].
Mwaka [[985]] Mwiceland aligundua njia ya kufika [[Greenland]] na baadaye [[Amerika ya Kaskazini]]. Mviking "[[Erik Mwekundu]]" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwa [[mwuaji]]. Alielekea [[magharibi]] kwa [[jahazi]] yake na kufika kwanza Greenland halafu [[pwani]] ya [[Kanada]] ya leo. Aliita bara jipya "nchi ya [[mzabibu]]" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila ma[[tunda]].


===Chini ya Norwei na Denmark===
Tangu [[1262]] uhuru wa Iceland ulikwisha kwa sababu viongozi walijiunga na [[Ufalme wa Norwei]]. Iceland iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali - hasa kwa sababu [[usafiri]] uliendelea kuwa mgumu - lakini mabwana wakuu walikuwa sasa wafalme wa Skandinavia, kwanza Wanorwei, baadaye Wa[[denmark]].
Tangu [[1262]] uhuru wa Iceland ulikwisha kwa sababu viongozi walijiunga na [[Ufalme wa Norwei]]. Iceland iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali - hasa kwa sababu [[usafiri]] uliendelea kuwa mgumu - lakini mabwana wakuu walikuwa sasa wafalme wa [[Skandinavia]], kwanza Wanorwei, baadaye Wa[[denmark]].


Mwaka [[1918]] [[Denmark]] ilirudisha madaraka yote ya serikali kwa Waiceland wenyewe isipokuwa mfalme wa Denmark aliendelea kama Mkuu wa nchi.
Mwaka [[1918]] [[Denmark]] ilirudisha madaraka yote ya [[serikali]] kwa Waiceland wenyewe isipokuwa mfalme wa Denmark aliendelea kama Mkuu wa nchi.


===Kuanzia uhuru===
Wakati wa [[Vita Kuu ya Dunia ya Pili]] Denmark ilivamiwa na [[Ujerumani]] na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka [[1944]] Iceland ilipata uhuru kamili.
Wakati wa [[Vita Kuu ya Dunia ya Pili]] Denmark ilivamiwa na [[Ujerumani]] na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka [[1944]] Iceland ilipata [[uhuru]] kamili.


Baada ya vita Iceland ilikuwa nchi mwanachama ya [[NATO]] lakini haina wanajeshi hadi leo. Ilifanya [[mkataba]] na [[Marekani]] ya kuwa Waamerika wanapewa haki ya kutumia kituo cha ndege kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Iceland.
Baada ya [[vita]] kwisha Iceland ilipata kuwa nchi mwanachama ya [[NATO]] lakini haina [[wanajeshi]] hadi leo. Ilifanya [[mkataba]] na [[Marekani]] ya kuwa Wamarekani wanapewa [[haki]] ya kutumia kituo cha [[Ndege (uanahewa)|ndege]] kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Iceland.


== Miji ==
== Miji ==

Pitio la 13:09, 19 Februari 2018

Isilandi
Ramani ya Iceland

Iceland (pia: Aisilandi, Isilandi; Kiiceland: "Nchi ya barafu") ni nchi ya Ulaya kwenye kisiwa cha Bahari ya Atlantiki ya kaskazini. Iko km 300 kutoka Greenland upande wa magharibi na km 1000 kutoka Norwei upande wa mashariki.

Eneo lake ni km² 103,000 lakini idadi ya watu ni laki tatu pekee.

Ingawa Iceland si sehemu ya rasi ya Skandinavia, inahesabiwa kati ya nchi za Skandinavia.

Jiografia

Vatnajökull ni barafuto kubwa kabisa ya Ulaya

Iceland ina asili ya kivolkeno. Ni kisiwa kikubwa cha safu ya mgongo kati wa Atlantiki mahali ambako mabamba ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya-Asia yanakutana. Kwa sababu hiyo kuna milima mingi, hasa volkeno ni nyingi. Kati ya volkeno mashuhuri za Iceland kuna Hekla, Eldgjá, Herðubreið na Eldfell.

Kwa ujumla hali ya hewa ni baridi na barafuto zinafunika sehemu kubwa ya nchi. Hasa nyanda za juu ni baridi mno, hivyo hakuna mimea. Karibu makazi yote ya watu ni karibu na pwani.

Kusini mwa kisiwa haikuwa baridi mno kwa sababu ya mkondo wa ghuba linaloendelea kusukuma maji ya ghuba la Mexiko hadi Atlantiki ya kaskazini. Mkondo huo unapofikia Iceland si ya moto tena lakini vuguvugu kidogo hivyo inazuia baridi kali sana.

Volkeno zimesababisha kuwepo kwa maji ya moto mahali pengi. Waiceland wanapenda kuogelea nje katika mabwawa hata wakati wa theluji katika maji ya moto kutokana na joto la kivolkeno. Joto hilo linatumika kidogo hata kwa kilimo; linapasha moto nyumba za kioo na kuwezesha mimea kuzaa matunda mwaka wote, hata wakati wa baridi kali. Kwa njia hiyo Iceland inavuna ndizi na machungwa yake!

Historia

Historia ya awali

Iceland iko mbali na bara la Ulaya na la Amerika tena katika mazingira ya baridi. Hivyo inaaminika haikuwa na watu kabisa hadi mwaka 800 BK. Wataalamu hawakubaliani kama ni mabaharia kutoka Norwei au Eire waliobahatika kufika kisiwani na kujenga makao ya kwanza.

Hakika waliofika wengi kidogo walikuwa Waviking au Wanorwei wa kale katika karne ya 9. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwa jina alikuwa Flóki Vilgerðarson.

Waviking waliofika walikuja pamoja na familia na watumishi au watumwa wao. Mnamo mwaka 930 machifu na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina ya katiba kwa Iceland. Walianzisha bunge la Althing. Ulikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa na cheo cha kuunganisha madaraka ya chifu, hakimu na kuhani. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Iceland ni nchi ya pekee ambako utaratibu wa kidemokrasia wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi ya wafalme au watawala wengine iliongezeka na kumeza haki zote za watu wa kawaida.

Mwaka 985 Mwiceland aligundua njia ya kufika Greenland na baadaye Amerika ya Kaskazini. Mviking "Erik Mwekundu" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwa mwuaji. Alielekea magharibi kwa jahazi yake na kufika kwanza Greenland halafu pwani ya Kanada ya leo. Aliita bara jipya "nchi ya mzabibu" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila matunda.

Chini ya Norwei na Denmark

Tangu 1262 uhuru wa Iceland ulikwisha kwa sababu viongozi walijiunga na Ufalme wa Norwei. Iceland iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali - hasa kwa sababu usafiri uliendelea kuwa mgumu - lakini mabwana wakuu walikuwa sasa wafalme wa Skandinavia, kwanza Wanorwei, baadaye Wadenmark.

Mwaka 1918 Denmark ilirudisha madaraka yote ya serikali kwa Waiceland wenyewe isipokuwa mfalme wa Denmark aliendelea kama Mkuu wa nchi.

Kuanzia uhuru

Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Denmark ilivamiwa na Ujerumani na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka 1944 Iceland ilipata uhuru kamili.

Baada ya vita kwisha Iceland ilipata kuwa nchi mwanachama ya NATO lakini haina wanajeshi hadi leo. Ilifanya mkataba na Marekani ya kuwa Wamarekani wanapewa haki ya kutumia kituo cha ndege kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Iceland.

Miji

Mji wa Reykyavik

Reykjavík ni mji mkuu wa Iceland pia bandari kubwa na kitovu cha uchumi na utamaduni wa nchi.

Miji mingine ni pamoja na Akureyri, Kópavogur, Hafnarfjördhur, Keflavík na Vestmannaeyjar.

Wakazi

Watu wa Iceland karibu wote (92.61%) ni Waskandinavia. Kati ya wengine, Wapolandi ndio wengi (3.36%).

Lugha ya Kiiceland bado inafanana sana na ile ya Kinorwei cha kale kilicholetwa kisiwani na wakazi wa kwanza miaka 1000 iliyopita. Watu bado wanaelewa mashairi yaliyotunzwa tangu zamani ile.

Kanisa la kitaifa la Kilutheri ni dini rasmi ya nchi. Hivyo Waiceland wengi (73.8%) wanahesabiwa kuwa Wakristo Walutheri, ingawa wengi hawafuati dini. Wakristo wa madhehebu mengine, kama vile Wakatoliki, wanafikia 11.7%. Kuna wafuasi wachache sana wa imani nyingine mbalimbali. Kwa jumla Iceland ni kati ya nchi ambazo zina wakazi wengi wasiomuamini Mungu.

Utamaduni

Hadi leo Waiceland hawana majina ya pili au ya familia. Kila mtoto anapewa jina lake la kwanza halafu jina la baba - wakati mwingine pia jina la mama. Kama mtoto ni wa kiume "-son" (=mwana) itaongezwa, kama ni binti "-dottir" (binti).

Kwa mfano mwimbaji mashuhuri wa kike Björk Guðmundsdóttir alipewa jina la "Björk". Baba yake alikuwa Guðmund hivyo anatumia jina hili pamoja na "-dottir": Guðmundsdottir: "Björk binti Guðmund". Kama mwenyewe atamzaa binti anaweza kuitwa "Björkdottir" lakini mara nyingi jina la baba hutumiwa. Wanawake wanaendelea na jina hili, hawaliachi wakati wa kuolewa.

Tazama pia

Marejeo

  • Jonsson, Asgeir (2008). Why Iceland? How One of the World's Smallest Countries Became the Meltdown's Biggest Casualty. McGraw–Hill Professional. ISBN 978-0-07-163284-3. 
  • Jonsson, Ivar (2012) 'Explaining the Crisis of Iceland – A Realist Approach' in Journal of Critical Realism, 11,1.
  • Heiðarsson, Jakob Oskar (2015) 'Iceland - My Small Island'.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Isilandi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.