Mtemi Mirambo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[image:Mirambo.jpg|thumb|[[Mchoro]] kutoka [[kitabu]] cha James William Buels kuhusu "Mashujaa wa Afrika" ([http://1890 1890])]]
[[image:Mirambo mnamo 1880.png|thumb|Mirambo katika miaka ya 1880, kabla ya kifo chake]]
'''Mtemi Mirambo''' ([[1840]]-[[1884]]) alikuwa [[mfalme]] wa [[Wanyamwezi]] katika [[magharibi]] ya [[Tanzania]] ya leo.
'''Mtemi Mirambo''' ([[1840]]-[[1884]]) alikuwa [[mtemi]] wa [[Wanyamwezi]] katika [[magharibi]] ya [[Tanzania]] ya leo.


[[Jina]] lake la awali lilikuwa "Mtyela Kasanda", lakini ni maarufu zaidi kama'''Mirambo''' (yaani "maiti nyingi").
[[Jina]] lake la awali lilikuwa "Mteyla Kasanda", lakini alikuwa maarufu zaidi kama '''Mirambo''' (yaani "maiti nyingi"). Alizaliwa kama mwana wa mtemi wa Uyowa, moja kati ya maeneo madogo ya Unyamwezi akarithi utemi kutoka babake mnamo mwaka 1860.


Mirambo aliwahi kutajirika kama [[mfanyabiashara]] ya [[pembe za ndovu]] na [[watumwa]] kwa njia ya [[Biashara ya misafara|misafara]] kati ya [[pwani]] ya [[Bahari Hindi]] na [[Kongo]].
Mirambo alitajirika kama [[mfanyabiashara]] ya [[pembe za ndovu]] na [[watumwa]] kwa njia ya [[Biashara ya misafara|misafara]] kati ya [[pwani]] ya [[Bahari Hindi]] na [[Kongo]].


Alitumia sehemu kubwa ya [[utajiri]] wake kujenga [[jeshi]] la binafsi. Kwa kusudi hilo alinunua [[bunduki]] aina ya [[gobori]] na kukusanya [[vijana]] wengi walioitwa "rugaruga". [[Rugaruga]] hao walihofiwa kote. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa [[pombe]] na [[bangi]] kwa kusudi la kuongeza ukatili na kupunguza [[hofu]] yao ya kifo.
Alitumia sehemu kubwa ya [[utajiri]] wake kujenga [[jeshi]] la binafsi. Kwa kusudi hilo alinunua [[bunduki]] aina ya [[gobori]] na kukusanya [[vijana]] wengi walioitwa "rugaruga". [[Rugaruga]] hao walihofiwa kote. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa [[pombe]] na [[bangi]] kwa kusudi la kuongeza ukatili na kupunguza [[hofu]] yao ya kifo.

Pitio la 01:53, 6 Februari 2018

Mirambo katika miaka ya 1880, kabla ya kifo chake

Mtemi Mirambo (1840-1884) alikuwa mtemi wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo.

Jina lake la awali lilikuwa "Mteyla Kasanda", lakini alikuwa maarufu zaidi kama Mirambo (yaani "maiti nyingi"). Alizaliwa kama mwana wa mtemi wa Uyowa, moja kati ya maeneo madogo ya Unyamwezi akarithi utemi kutoka babake mnamo mwaka 1860.

Mirambo alitajirika kama mfanyabiashara ya pembe za ndovu na watumwa kwa njia ya misafara kati ya pwani ya Bahari Hindi na Kongo.

Alitumia sehemu kubwa ya utajiri wake kujenga jeshi la binafsi. Kwa kusudi hilo alinunua bunduki aina ya gobori na kukusanya vijana wengi walioitwa "rugaruga". Rugaruga hao walihofiwa kote. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa pombe na bangi kwa kusudi la kuongeza ukatili na kupunguza hofu yao ya kifo.

Kwa kawaida vijana hao walikuwa wanaume walioishi bila ukoo na bila familia kisha kutoroka kwenye hali ya utumwa au kuwa wapagazi wa misafara.[1][2] Mirambo aliwapokea na kuwapa silaha na kwa njia hii alishinda maadui na aliweza kupanua eneo lake hadi kuwa mtemi mkuu wa Wanyamwezi[3][4] kuanzia mwaka 1860 hadi kifo chake mnamo 1884[5].

Alisifiwa na Henry Morton Stanley kama "Napoleon Bonaparte Mwafrika" kutokana na ushujaa wake dhidi ya Waarabu waliomuunga mkono Stanley mwenyewe. Hata hivyo hakufaulu kuteka Tabora kutoka mikononi mwao.

Tanbihi

  1. John Iliffe: A Modern History of Tanganyika. Cambridge University Press, Cambridge 1979, uk. 64
  2. The Cambridge History of Africa, vol. 6
  3. The Nyamwezi aristocracy was appalled when someone who was not royalty took over the religiously ceremonial office of ntemi.
  4. The Cambridge History of Africa, vol. 5
  5. It is possible that he was strangled to death, since an old Nyamwezi custom was to strangle their mtemi when they became unfit to rule.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtemi Mirambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.