Mshale (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Kipala moved page Kausi to Kausi (kundinyota) over redirect
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
<sup>Kwa habari za sayari ya nane katika mfumo wa jua letu (wakati mwingine kwa kosa huitwa pia "Kausi") angalia hapa [[Neptun]]; kwa matumizi mengine ya jina "Sagittarius" angalia hapa [[Sagittarius]]</sup>
<sup>Kwa habari za sayari (wakati mwingine kwa kosa huitwa pia "Kausi") angalia hapa [[Neptun]]; kwa matumizi mengine ya jina "Sagittarius" angalia hapa [[Sagittarius]]</sup>


[[Picha:Kausi Sagittarius.jpg|thumb|400px|Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)]]
[[Picha:Kausi Sagittarius.jpg|thumb|400px|Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)]]

Pitio la 10:06, 7 Novemba 2017

Kwa habari za sayari (wakati mwingine kwa kosa huitwa pia "Kausi") angalia hapa Neptun; kwa matumizi mengine ya jina "Sagittarius" angalia hapa Sagittarius

Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)
Kausi (sagittarius) jinsi anavyochorwa na msanii

Kausi (pia Mshale au Sagittarius[1] kwa Kilatini/Kiingereza) ni jina la kundinyota kwenye zodiaki.

Nyota za Kausi huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Kausi" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Jina

Jina la Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu Kaus قوس linalomaanisha "upinde", maana hii ni karibu sawa na jina la Kilatini "sagittarius" (mpiga upinde). Wataalamu wa kale waliona katika nyota zake picha ya mtu anayekalia juu ya farasi akishika pinde na kulenga mshale.

Jina la "Kaus" limetumiwa pia katika astronomia ya kimagharibi kutaja nyota kadhaa zilizomo hapa kama vile Kaus Australis, Kaus Medius na Kaus Borealis.

Katika vitabu kadhaa vya shule za msingi nchini Tanzania "Kausi" imetumiwa kwa kosa kutaja sayari ya nane katika mfumo wa jua letu yaani Neptun.

Kuonekana

Kausi inaonekana pale angani ambako njia nyeupe inang'aa zaidi yaani kuelekea kitovu cha galaksi yetu.

Kausi ni kati ya fungunyota zilizojulikana tangu karne nyingi zikitumiwa hasa na mabaharia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.

Sifa za pekee

Katika eneo la Kausi wanaastronomia walitambua magimba ya angani kadhaa ya maana. Hizi ni pamoja na

  • Alfa Sagittarii ambayo ni chanzo cha mawimbi ya redio; inaaminiwa ya kwamba mawimbi haya ni dalili za kuwepo kwa shimo cheusi kubwa sana
  • Nebula kadhaa zilizoandikishwa katika orodha ya Messier kama vile nebula za lagoon, omega na red spider.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Sagittarius" katika lugha ya Kilatini ni "Sagittarii" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Sagittarii, nk.

Marejeo

  • kuhusu jina: Jan Knappert, The Swahili names of stars, planets and constellations; makala katika jarida la The Indian Ocean Review, Perth, Australia September 1993, uk. 7