Turkmenistan : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
→‎Tanbihi: +kiungo cha orodha ya lugha
Mstari 100: Mstari 100:
Wakazi walio wengi ni [[Waislamu]]; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 87 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli [[dini]] yao. Wakristo ni 9%, hasa [[Waorthodoksi]].
Wakazi walio wengi ni [[Waislamu]]; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 87 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli [[dini]] yao. Wakristo ni 9%, hasa [[Waorthodoksi]].


==Tazama Pia==
==Tazama pia==
*[[Orodha ya lugha za Turkmenistan]]
* [[Orodha ya lugha za Turkmenistan]]
* [[Orodha ya nchi kufuatana na wakazi]]


==Tanbihi==
==Tanbihi==

Pitio la 10:29, 30 Oktoba 2017

Turkmenistan


Turkmenistan ni nchi ya Asia ya Kati.

Jina limetokana na lugha ya Kiajemi; lamaanisha "nchi wa Waturkmeni".

Imepakana na Afghanistan, Uajemi, Uzbekistan, Kazakhstan na Bahari Kaspi.

Jiografia

Ramani ya Turkmenistan.

Nchi ina eneo la km² 488,100, karibu sawa na Kamerun.

Sehemu kubwa (80 %) ni jangwa, hasa jangwa Karakum.

Milima ya Kopet Dag kusini magharibi inafikia kimo cha mita 2,912.

Kati ya mito mikubwa ni Amu Darya, mto Murghab na mto Hari Rud.

Hali ya hewa si baridi sana lakini kuna joto kali wakati wa kiangazi.

Mvua ni chache; zanyesha hasa kati ya Januari na Mei.

Miji muhimu ni Ashgabat, Turkmenbashi (zamani Krasnovodsk) na Dashoguz.

Historia

Turkmenistan ilitwaliwa na Urusi tangu mwisho wa karne ya 19 ikaingia hivyo katika Umoja wa Kisovyeti baada ya mwaka 1917 na kuwa jamhuri ndani yake.

Hadi mwaka 1991 ilikuwa jamhuri ya Umoja wa Kisovyet kwa jina la Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiturkmeni.

Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti kiongozi wa chama cha kikomunisti Saparmirat Niyasov akaendelea kushika uongozi akitawala kama rais hadi kifo chake mwaka 2006.

Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake mwenyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Turkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchiniː mara nyingi sanamu za dhahabu hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu.

Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli zilimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko makubwa jinsi ilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti penginepo.

Zaidi ya nusu ya wananchi hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini, lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya chini sana, lakini kuna uhaba wa mara kwa mara.

Baada ya kifo cha Niyasov kamati ya viongozi ilimteua makamu wa waziri mkuu Gurbanguly Berdimuhammedov kuwa rais mpya ingawa kikatiba mwenyekiti wa bunge alitakiwa kuchukua nafasi hii.

Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mahakamani juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithibitishwa katika uchaguzi wa tarehe 11 Februari 2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.

Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulifanyika uchaguzi wa vyama vingi.

Watu

Waturkmeni wenyewe ni 85% za wakazi wote, wakifuatwa na Wauzbeki (5%) na Warusi (4%).

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiturkmeni (72%). Kinafuata Kirusi (12%).

Wakazi walio wengi ni Waislamu; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 87 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli dini yao. Wakristo ni 9%, hasa Waorthodoksi.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Brummel, Paul (2006). Bradt Travel Guide: Turkmenistan. Bradt Travel Guides. ISBN 978-1841621449. 
  • Abazov, Rafis (2005). Historical Dictionary of Turkmenistan. Scarecrow Press. ISBN 978-0810853621. 
  • Clammer, Paul; Kohn, Michael; Mayhew, Bradley (2014). Lonely Planet Guide: Central Asia. Lonely Planet. ISBN 978-1741799538. 
  • Hopkirk, Peter (1992). The Great Game: The Struggle for Empire in Central Asia. Kodansha International. ISBN 978-1568360225. 
  • Blackwell, Carole (2001). Tradition and Society in Turkmenistan: Gender, Oral Culture and Song. Routledge. ISBN 978-0700713547. 
  • Kaplan, Robert (2001). Eastward to Tartary: Travels in the Balkans, the Middle East, and the Caucasus. Vintage. ISBN 978-0375705762. 
  • Kropf, John (2006). Unknown Sands: Journeys Around the World's Most Isolated Country. Dusty Spark Publishing. ISBN 978-0976356516. 
  • Rall, Ted (2006). Silk Road to Ruin: Is Central Asia the New Middle East?. NBM Publishing. ISBN 978-1561634545. 
  • Theroux, Paul (28 May 2007). The Golden Man: Saparmurat Niyazov’s reign of insanity..
  • Vilmer, Jean-Baptiste (2009). Turkménistan (in French). Editions Non Lieu. ISBN 978-2352700685. 

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Vingine
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Turkmenistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.