Shairi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
/* (i) Mashairi ya kimapokeo
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 24: Mstari 24:
===(i) Mashairi ya kimapokeo===
===(i) Mashairi ya kimapokeo===
Vilevile huitwa ''mashairi funge'' - ni mashairi yanayozingatia kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila [[ubeti]] na kituo katika shairi.
Vilevile huitwa ''mashairi funge'' - ni mashairi yanayozingatia kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila [[ubeti]] na kituo katika shairi.

===(ii) Mashairi ya kimamboleo===
===(ii) Mashairi ya kimamboleo===
Haya ni mashairi yasiyozingatia kanuni za kimapokeo, yaani, hayazingatii kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila ubeti na kituo katika shairi.
Haya ni mashairi yasiyozingatia kanuni za kimapokeo, yaani, hayazingatii kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila ubeti na kituo katika shairi.

Pitio la 18:48, 26 Septemba 2017

Shairi ni sehemu ya fasihi. Mashairi ni tungo zenye kutumia mapigo ya silabi kwa utaratibu maalumu wa kimuziki kwa kutumia lugha ya mkato, lugha ya picha na tamathali za semi.

Mashairi huweza kuandikwa au kutungwa kulingana na jinsi yanavyoonekana. hii ina maana kuwa, mashairi huweza kutofautishwa kwa idadi ya mishororo, jinsi maneno yalivyopangwa, urari wa vina na kadhalika.

Kuna mashairi yanayofuata taratibu za kimapokeo, yaani yanazingatia taratibu za urari na vina, mizani, idadi sawa ya mistari, vituo na beti.

Mashairi huwa na mizani 14 au 16 katika kila mstari, yaani mizani 7 au 8 kwa kila kipande cha mstari.

Pia kuna mashairi yasiyofuata utaratibu huo wa kimapokeo na huitwa mashairi ya kimamboleo. Mashairi haya mara nyingi huwa ni nyimbo.

Mfano
  • Tulopeleka bungeni, wamegeuka nyang'au,
  • Mafisadi kama nini, baladhuli mabahau,
  • Wanavunja mpini, konde wamelisahau,
  • Zamani na siku hizi, mambo sivyo yavyokuwa.
  • Mwalimu mwana elimu, asiyekujua ni nani?
  • Kwake ilete elimu, liyopewa na Maanani,
  • Watu wote wafahamu, hapingiki hasilani,
  • Adharauye mwalimu, kapungua akilini.

Aina za mashairi

Kuna aina kuu mbili za mashairi, nazo ni kama zifuatavyo:

(i) Mashairi ya kimapokeo

Vilevile huitwa mashairi funge - ni mashairi yanayozingatia kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila ubeti na kituo katika shairi.

(ii) Mashairi ya kimamboleo

Haya ni mashairi yasiyozingatia kanuni za kimapokeo, yaani, hayazingatii kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila ubeti na kituo katika shairi. Mashairi haya pia huitwa mashairi huru/mashairi ghuni/mashairi ya kisasa/masivina/mapingiti.

Mizani

Mizani ni ulinganifu wa idadi ya silabi katika kila kipande au mistari ya ubeti wa shairi. Mara nyingi mashairi ya kimapokeo huwa na mizani nane (8) kwa kila kipande na mizani kumi na sita (16) kwa kila mstari (mshororo).

Vina

Vina ni silabi zenye sauti ya namna moja zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mshororo wa kila ubeti wa shairi. Hivyo basi kuna vina vya kati na vina vya mwisho.

Ubeti

Ni fungu la mistari lenye maana kamili. Ubeti unaweza kulinganishwa na aya katika maandiko ya kinathari. Mara nyingi ubeti huishia katika kituo. Ubeti mmoja unaweza kuwa na:

  • Mstari mmoja (tamonitha)
  • Mistari miwili (tathiniya/tathinia/uwili): shairi hili huwa na mishororo miwili katika kila ubeti. vina vyake vyaweza kuwa na mtiririko.
  • Mistari mitatu (tathilitha): shairi hili huwa na mishororo mitatu katika kila ubeti. vina vyake huenda vikawa na urari.
  • Mistari mine (tarbia): shairi la aina hii huwa na mishororo minne katika kila ubeti. mara nyingi shairi hili hugawanywa katika sehemu mbili, ukwapi na utao. mshororo wa kwanza wa shairi hili huitwa kipokeo, wa pili huitwa mloto, wa nne huitwa kibwagizo. kibwagizo huwa kinarudiwarudiwa katika kila ubeti.
  • Mistari mitano (takhmisa): hili ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti
  • Mistari zaidi ya mitano (sabilia), kwa mfano: tasdisa huwa na mishororo sita katika kila ubeti, tathmina huwa na mishororo minane katika kila ubeti, ukumi huna na mishororo kumi katika kila ubeti.

Aina za mashairi jinsi yanavyojitokeza

  1. Kikwamba ni aina ya shairi lililo na kibwagizo ambacho ni kifupi ukilinganisha na ile mishororo mingine. hili huweza kuuchukuwa mfumo wa mashairi yale mengine.
  2. Ngonjera: shairi hili huhusisha waimbaji zaidi ya mmoja ambao uimbaji wao huwa katika mfumo wa majibizano.

Kituo

Ni mstari (mshororo) wa mwisho katika kila ubeti wa shairi ambao huonesha msisitizo wa ubeti mzima au shairi zima. Wakati mwingine kituo huitwa kibwagizo/korasi/mkarara/kiitikio.

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shairi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.