Mwangaza unaoonekana : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 10: Mstari 10:
Kwa kutaja kiasi cha uangavu wanaastronomia hutumia kizio cha "magnitudo" (kifupi mag). Neno hili la [[Kilatini]] linamaanisha "ukubwa". Kadri uangavu ni mkubwa namba ya magnitudo ni ndogo.
Kwa kutaja kiasi cha uangavu wanaastronomia hutumia kizio cha "magnitudo" (kifupi mag). Neno hili la [[Kilatini]] linamaanisha "ukubwa". Kadri uangavu ni mkubwa namba ya magnitudo ni ndogo.


Kwa mfano nyota ya [[Sumbula]] ina magnitudo ya +1,04 mag. [[Rijili ya Jabari]] inayojulikana pia kama [[en:Rigel|Rigel]] ina uanganvu unaoonekana wa +0.12 mag maana yake nuru yake ni kali zaidi.
Kwa mfano nyota ya [[Sumbula]] ina magnitudo ya +1,04 mag. [[Rijili ya Jabari]] inayojulikana pia kama [[:en:Rigel|Rigel]] ina uanganvu unaoonekana wa +0.12 mag maana yake nuru yake ni kali zaidi.


Kama gimba la anga inang'aa sana ina [[namba hasi]] kwa mfano nyota angavu sana kama [[Shira]] ''(Sirius)'' na [[sayari]] za [[Zuhura]] ''(Venus)'' au [[Mshtarii]] ''(Jupiter)''.
Kama gimba la anga inang'aa sana ina [[namba hasi]] kwa mfano nyota angavu sana kama [[Shira]] ''(Sirius)'' na [[sayari]] za [[Zuhura]] ''(Venus)'' au [[Mshtarii]] ''(Jupiter)''.

Pitio la 20:57, 20 Julai 2017

Uangavu ni tabia ya nyota inayosaidia kuzitofautisha. Kuna tofauti kati ya uangavu unaoonekana na uangavu halisi.

Umbali kati ya vitu kwenye anga la nje ni kubwa sana. Nyota kubwa kama iko mbali inaonekana hafifu, nyota ndogo kama iko karibu inaonekana angavu sana.

  • Uang‘avu unaoonekana ni kipimo cha ukali wa nuru wa gimba la angani jinsi unavyoonekana kwa mtazamaji kwenye dunia yetu. Unatajwa kwa namba na kizio chake ni magnitudo, kifupi mag. Kadri uang‘avu ni juu namba yake ni ndogo. [1] Kitu ang‘avu zaidi angani ni jua letu kenye uang‘avu unaonekana wa -−26,73 mag. Nyota ya Rijili Kantori ( en:Alpha Centauri) inaonekana ang‘avu kushinda nyota kubwa zaidi ya Jibuta la Jauza kwa sababu iko karibu zaidi na dunia.
  • Uang‘avu' halisi ni kipimo cha ukali wa nuru jinsi ingeonekana kwa mtazamji aliyeko katika umbali wa miaka ya nuru 32.6[2][3] Kipimo hiki kinawaruhusu wanaastronomia kulinganisha uang‘avu wa magimba kwa kutumia umbali sanifu.

Kipimo cha magnitudo

Kwa kutaja kiasi cha uangavu wanaastronomia hutumia kizio cha "magnitudo" (kifupi mag). Neno hili la Kilatini linamaanisha "ukubwa". Kadri uangavu ni mkubwa namba ya magnitudo ni ndogo.

Kwa mfano nyota ya Sumbula ina magnitudo ya +1,04 mag. Rijili ya Jabari inayojulikana pia kama Rigel ina uanganvu unaoonekana wa +0.12 mag maana yake nuru yake ni kali zaidi.

Kama gimba la anga inang'aa sana ina namba hasi kwa mfano nyota angavu sana kama Shira (Sirius) na sayari za Zuhura (Venus) au Mshtarii (Jupiter).

Kipimo hakifuati mstari bali vizio vyake vinafuatana kwa hatua za logi. kwa hiyo ongezeko la uangavu kutoka kizio kimoja hadi kile kidogo zaidi kinachofuata ni takriban mara 2.5

Historia ya kipimo

Chanzo cha vipimo hivi ni kazi ya Hipparchos wa Nikaia mtaalamu wa Ugiriki ya Kale. [4] Aliorodhesha nyota kufuatana na uanganvu akazipanga nyota angavu zaidi kwenye daraja la kwanza, zile zilizonekana hafifu zaidi katika madaraja ya pili, tatu na kadhalika hadi daraja la sita. Orodha yake ilikuwa msingi wa kitabu mashuhuri cha Almagest cha Klaudio Ptolemaio kilichoendelea kuwa msingi wa utaalamu wa nyota hadi mwisho wa karne za kati.

Baadaye skeli ya kale ilipanushwa pande zote mbili kwa kupokea pia magimba angavu zaidi au hafifu zaidi. Kufuatana na ufafanuzi wa mwaka 1850 ungavu wa nyota ya daraja la kwanza (1.0 mag) ni mara 100 uangavu wa nyota ya 6.0 mag, na hiyo mara 100 kuliko nyota ya 11.0 mag.

Mifano ya uangavu unaoonekana na halisi

Nyota Uangavu
unaoonekana
(m)
Uangavu
halisi
(M)
Umbali[5]
Jua −26,73 mag 0+4,84 mag 4,851·10−6 pc
Shira
(en:Sirius)
0−1,46 mag 0+1,43 mag 2,64 pc
Vega
0+0,03 mag 0+0,58 mag 7,75 pc
Sumbula
(en:Spica)
0+1,04 mag 0−3,51 mag 81,3 pc
Rijili ya Jabari
(en:Rigel)
0+0,12 mag 0−6,78 mag 240 pc
Dhanabu
(en:Deneb)
0+1,25 mag 0−7,24 mag 499 pc

Marejeo

  1. Robert Bruce Thompson; Barbara Fritchman Thompson, Astronomy Hacks (Sebastopol, CA: O'Reilly, 2005), p. 88
  2. Rony De Laet, The Casual Sky Observer's Guide: Stargazing with Binoculars and Small Telescopes (New York: Springer, 2012), p. 29
  3. Umbali huu ni sawa na parsec 10
  4. Leila Belkora, Minding the Heavens: The Story of our Discovery of the Milky Way (Bristol: Institute of Physics, 2003), pp. 19–20
  5. Umbali katika astronomia mara nyingi hutajwa kwa parsec; kizio hiki ni sawa na miaka ya nuru 3.26