Kaa (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:CancerCC.jpg|thumb|300px|Nyota kuu za Saratani (Cancer) jinsi zinavyoonekana angani. <br/> <small>Mistari imeongezwa kwenye picha tu</small>]]
[[Picha:Saratani Cancer.jpg|thumb|400px|Nyota kuu za Saratani (Cancer) jinsi zinavyoonekana angani. <br/> <small>Mistari imeongezwa kwenye picha tu</small>]]
[[Picha:Cancer constellation map.png|350px|thumb|Ramani ya kundinyota Saratani]]
[[Picha:Cancer constellation map.png|350px|thumb|Ramani ya kundinyota Saratani]]
'''Saratani''' ni [[kundinyota]] ya [[zodiaki]] inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la [[:en:Cancer (constellation)|Cancer]]<ref>[[Uhusika milikishi]] ''([[:en:genitive]])'' ya neno "Cancer" katika lugha ya [[Kilatini]] ni "Cancris" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Cancris, nk.</ref>. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] <ref>[https://www.iau.org/public/themes/constellations/ The Constellations], tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017</ref>

Pitio la 11:01, 19 Julai 2017

Nyota kuu za Saratani (Cancer) jinsi zinavyoonekana angani.
Mistari imeongezwa kwenye picha tu
Ramani ya kundinyota Saratani

Saratani ni kundinyota ya zodiaki inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Cancer[1]. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2]

Jinsi ilivyo kwenye kundinyota zote, nyota za Saratani hazikai pamoja hali halisi katika anga la nje lakini zinaonekana vile tu kutoka duniani. Hali halisi kuna umbali mkubwa kati yao. Kwa hiyo "Saratani" inataja eneo la angani jinsi inavyoonekana kutoka dunia.

Jina

Jina la Kiswahili ni Saratani latokana na Kiarabu سرطان sartan linalomaanisha kaa. Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Καρκίνος karnikos kwa maana hiyohiyo na hao walipokea tayari kundinyota hii kutoka Babeli lakini Wabebli waliiona kama alama ya kobe ya maji.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Saratani" limesahauliwa ikiwa kundinyota inaitwa kwa tafsiri tu "Kaa".

Katika vitabu kadhaa vya shule jina la Saratani limetumiwa kutaja sayari ya Zohali kwa kulichanganya na matamshi ya jina la Kiingereza "Saturn".

Mahali pake

Saratani iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Jauza (Gemini) upande wa magharibi na Asadi (Leo) upande wa mashariki.

Magimba ya angani

Saratani haina nyota angavu sana si rahisi kuiona. Nyota angavu zaidi ni Beta Cancri yenye uangavu unaoonekana wa 3.8 mag. Umbali wake na dunia ni miaka ya nuru 230. Kuna fungunyota moja inayoonekana kwa macho matupu hii ni M 44 inayoitwa pia Praesepe yenye uangavu unaoonekana wa 3.7 ikionekana kama doa dogo angavu.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Cancer" katika lugha ya Kilatini ni "Cancris" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Cancris, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017

Marejeo

  • Ian Ridpath and Wil Tirion (2007). Stars and Planets Guide, Collins, London. ISBN 978-0007251209. Princeton University Press, Princeton. ISBN 978-0-691-13556-4.
  • Dictionary of Symbols, by Carl G. Liungman, W. W. Norton & Company. ISBN 978-0-393-31236-2
  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 107 ff (online kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons