Mwangaza unaoonekana : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 44: Mstari 44:
|style="text-align:center"| 81,3 pc
|style="text-align:center"| 81,3 pc
|-
|-
|style="text-align:center"| [[Rijili Kantori]]</br> <small>([[:en:Alpha Centauri]])</small>
|style="text-align:center"| [[Rijili ya Jabari]]</br> <small>([[:en:Rigel]])</small>
|style="text-align:center"| {{0}}+0,12 mag
|style="text-align:center"| {{0}}+0,12 mag
|style="text-align:center"| {{0}}−6,78 mag
|style="text-align:center"| {{0}}−6,78 mag

Pitio la 10:42, 10 Julai 2017

Uangavu ni tabia ya nyota inayosaidia kuzitofautisha. Kuna tofauti kati ya uangavu unaoonekana na uangavu halisi.

Umbali kati ya vitu kwenye anga la nje ni kubwa sana. Nyota kubwa kama iko mbali inaonekana hafifu, nyota ndogo kama iko karibu inaonekana angavu sana.

  • Uang‘avu unaoonekana ni kipimo cha ukali wa nuru wa gimba la angani jinsi unavyoonekana kwa mtazamaji kwenye dunia yetu. Unatajwa kwa namba na kizio chake ni magnitudo, kifupi mag. Kadri uang‘avu ni juu namba yake ni ndogo. [1] Kitu ang‘avu zaidi angani ni jua letu kenye uang‘avu unaonekana wa -−26,73 mag. Nyota ya Rijili Kantori ( en:Alpha Centauri) inaonekana ang‘avu kushinda nyota kubwa zaidi ya Jibuta la Jauza kwa sababu iko karibu zaidi na dunia.
  • Uang‘avu' halisi ni kipimo cha ukali wa nuru jinsi ingeonekana kwa mtazamji aliyeko katika umbali wa miaka ya nuru 32.6[2][3] Kipimo hiki kinawaruhusu wanaastronomia kulinganisha uang‘avu wa magimba kwa kutumia umbali sanifu.

Kipimo cha magnitudo

Kwa kutaja kiasi cha uangavu wanaastronomia hutumia kizio cha "magnitudo" (kifupi mag). Neno hili la Kilatini linamaanisha "ukubwa". Kadri uangavu ni mkubwa namba ya magnitudo ni ndogo.

Kwa mfano nyota ya Sumbula ina magnitudo ya +1,04 mag. Rijili Kantori inayojulikana pia kama ambayo ni nyota jirani yetu katika anga la njke ina uanganvu unaoonekana wa +0.12 mag maana yake nuru yake ni kali zaidi.

Kama gimba la anga inang'aa sana ina namba hasi kwa mfano nyota angavu sana kama Shira (Sirius) na sayari za Zuhura (Venus) au Mshtarii (Jupiter).

Kipimo hakifuati mstari bali vizio vyake vinafuatana kwa hatua za logi. kwa hiyo ongezeko la uangavu kutoka kizio kimoja hadi kile kidogo zaidi kinachofuata ni takriban mara 2.5

Mifano ya uangavu unaoonekana na halisi

Nyota Uang‘avu
unaoonekana
(m)
Uang‘avu
halisi
(M)
Umbali[4]
Jua −26,73 mag 0+4,84 mag 4,851·10−6 pc
Shira
(en:Sirius)
0−1,46 mag 0+1,43 mag 2,64 pc
Vega
0+0,03 mag 0+0,58 mag 7,75 pc
Sumbula
(en:Spica)
0+1,04 mag 0−3,51 mag 81,3 pc
Rijili ya Jabari
(en:Rigel)
0+0,12 mag 0−6,78 mag 240 pc
Dhanabu
(en:Deneb)
0+1,25 mag 0−7,24 mag 499 pc

Marejeo

  1. Robert Bruce Thompson; Barbara Fritchman Thompson, Astronomy Hacks (Sebastopol, CA: O'Reilly, 2005), p. 88
  2. Rony De Laet, The Casual Sky Observer's Guide: Stargazing with Binoculars and Small Telescopes (New York: Springer, 2012), p. 29
  3. Umbali huu ni sawa na parsec 10
  4. Umbali katika astronomia mara nyingi hutajwa kwa parsec; kizio hiki ni sawa na miaka ya nuru 3.26