Wambunga : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 12: Mstari 12:
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{DEFAULTSORT:Mbunga}}
{{DEFAULTSORT:Mbunga}}
{{Makabila ya Tanzania}}

[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Wilaya ya Kilombero]]
[[Jamii:Wilaya ya Kilombero]]

Pitio la 13:32, 9 Julai 2017

Wambunga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi upande wa kaskazini wa Wapogolo, katika wilaya ya Kilombero (Ifakara), mkoani Morogoro. Lugha yao ni Kimbunga.

Historia

Wambunga ni kabila dogo lililotokana na Wangoni baada ya mfarakano wa viongozi wa makundi yao walioingia katika eneo la Tanzania ya leo. Hivyo basi Wambunga ni Wangoni maseko (mafiti) walioingia Tanganyika kupitia kusini mashariki mwa Ruvuma wakiongozwa na kiongozi wa Wangoni maseko Mputa.

Baada ya kutoelewana miongoni mwa makundi ya Wangoni kukapelekea chuki iliyosababisha viongozi wa makundi hayo kuuana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo Mputa akauawa, na mwanae Malunda akawa mtawala wa kundi hilo. Baadaye Malunda akawa na wasiwasi wa maisha yake kutokana na hali hiyo, hivyo akaamua kurudi na kundi la Wangoni maseko katika Zimbabwe ya leo walikotokea awali.

Lakini katika hilo baadhi yao waligoma kurudi Zimbabwe, ndipo baada ya Malunda kuondoka waliobaki wakahama pale Songea na kusogea mlima Mbunga ulioko pembezoni mwa mkoa wa Ruvuma. Baadaye, walipoona makundi ya Wangoni wakiendelea kupigana wao kwa wao, wakaamua kuondoka hapo mlima Mbunga na kuambaambaa Ulanga (leo katika mkoa wa Morogoro), hasa kwenye bonde la mto Kilombero.

Walijulikana kwa matamshi yao kuwa Wangoni, lakini wao walijiita Wambunga kwani wametokea mlima Mbunga. Hiyo ilitokana na kuchoshwa na vita, maana wote waliwatambua Wangoni kwa kupenda vita, kumbe kwa kusema hivyo wangebaki salama wenyeji wao wasiwadhuru, maana wakati huo Wangoni walishaanza uchokozi wa kivita na Muyugumba, kiongozi wa Wahehe.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wambunga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.