Mshale (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3: Mstari 3:
[[Picha:SagittariusCC.jpg|thumb|Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)]]
[[Picha:SagittariusCC.jpg|thumb|Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)]]
[[Picha:Sidney Hall - Urania's Mirror - Sagittarius and Corona Australis, Microscopium, and Telescopium.jpg|thumb|Kausi (sagittarius) jinsi anavyochorwa na msanii]]
[[Picha:Sidney Hall - Urania's Mirror - Sagittarius and Corona Australis, Microscopium, and Telescopium.jpg|thumb|Kausi (sagittarius) jinsi anavyochorwa na msanii]]

'''Kausi''' ni jina la [[kundinyota]] inayojulikana pia kwa jina la Kilatini '''[[:en:Sagittarius (constellation)|Sagittarius]]'''.
'''Kausi''' ni jina la [[kundinyota]] kwenye [[zodiaki]] inayojulikana pia kwa jina la Kilatini '''[[:en:Sagittarius (constellation)|Sagittarius]]'''.


==Jina==
==Jina==

Pitio la 20:35, 28 Mei 2017

Kwa habari za sayari ya nane katika mfumo wa jua letu (wakati mwingine kuitwa "Kausi" pia) angalia hapa Neptun

Nyota za Kausi angani (mistari imeongezwa kwenye picha tu)
Kausi (sagittarius) jinsi anavyochorwa na msanii

Kausi ni jina la kundinyota kwenye zodiaki inayojulikana pia kwa jina la Kilatini Sagittarius.

Jina

Jina la Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu Kaus قوس linalomaanisha "upinde", maana karibu sawa na jina la Kilatini "sagittarius" (mpiga upinde). Wataalamu wa kale waliona katika nyota zake picha ya mtu anayekalia juu ya farasi akishika pinde na kulenga mshale.

Jina la "Kaus" limetumiwa pia katika astronomia ya kimagharibi kutaja nyota kadhaa zilizomo hapa kama vile Kaus Australis, Kaus Medius na Kaus Borealis.

Katika vitabu kadhaa vya shule za msingi nchini Tanzania "Kausi" imetumiwa kwa kosa kutaja sayari ya nane katika mfumo wa jua letu yaani Neptun.

Kuonekana

Kausi inaonekana pale angani ambako njia nyeupe inang'aa zaidi yaani kuelekea kitovu cha galaksi yetu.

Kausi ni kati ya fungunyota zilizojulikana tangu karne nyingi zikitumiwa hasa na mabaharia kutafuta njia baharini wakati wa usiku.

Sifa za pekee

Jinsi ilivyo kwenye kundinyota zote nyota za Kausi hazikai pamoja hali halisi lakini zinaonekana vile tu kutoka duniani. Hali halisi kuna umbali mkubwa kati yao. Kwa hiyo "Kausi" inataja eneo la angani jinsi inavyoonekana kutoka dunia.

Katika eneo la Kausi wanaastronomia walitambua magimba ya angani kadhaa ya maana. Hizi ni pamoja na

  • Sagittarius A ambayo ni chanzo cha mawimbi ya redio; inaaminiwa ya kwamba mawimbi haya ni dalili za kuwepo kwa shimo cheusi kubwa sana
  • Nebula kadhaa zilizoandikishwa katika orodha ya Messier kama vile nebula za lagoon, omega na red spider.

Marejeo

  • kuhusu jina: Jan Knappert, The Swahili names of stars, planets and constellations; makala katika jarida la The Indian Ocean Review, Perth, Australia September 1993, uk. 7