Unururifu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:ISO 7010 W003.svg|thumb|Tanganzo: Hapa kuna mnururisho hatari !]]
[[Picha:Alphadecay.jpg|thumb|Mbunguo nururifu wa vyembe vya α ]]
[[Picha:Alphadecay.jpg|thumb|Mbunguo nururifu wa vyembe vya α ]]
[[Picha:Betadecay.jpg|thumb|Mbunguo nururifu wa vyembe vya β]]
[[Picha:Betadecay.jpg|thumb|Mbunguo nururifu wa vyembe vya β]]

Pitio la 20:43, 21 Mei 2017

Tanganzo: Hapa kuna mnururisho hatari !
Mbunguo nururifu wa vyembe vya α
Mbunguo nururifu wa vyembe vya β

Unururifu (ing. radioactivity; pia: mbunguo nururifu ing. radioactive decay) ni tabia ya elementi kadhaa ambako kiini cha atomi si dhabiti bali inaweza kubadilika kuwa kiini cha atomi kingine na katika mchakato huu kinatoa mnururisho. Wakati wa badiliko atomi inatoa vyembe nyuklia. Mifano ya elementi ambazo si thabiti ni urani na plutoni.

Kuna pia hali za elementi kadhaa ambazo kwa kawaida ni thabiti lakini baada ya kupokea nyutroni ya nyongeza zinakuwa nururifu. Kwa mfano kuna kaboni ya kawaida inayoitwa 12C , hii ni thabiti. Lakini kuna pia kiwango kidogo cha 14C ambayo si thabiti ni nururifu; hali hii huitwa isotopi cha kaboni. Kaboni ya 14C inatengenezwa mfululizo katika tabaka za juu ya angahewa ya dunia ambako atomu za nitrojeni zinagongwa na miale ya jua na kupotea nyutroni; hizi nyutroni zinaweza kugongana tena na atomi ya nitrojeni na kujiunganisha naye na hivyo kuunda atomi ya 14C.

Tabia hii ya unururifu ilitambuliwa mara ya kwanza na Antoine Henri Becquerel mwaka 1896, halafu ni Marie Curie na Pierre Curie waliotunga neno "radioactivity" (=unururifi) kwa tabia hii. Wote watatu walipokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia kwa kazi hii mwaka 1903.

Mnururisho unaotoka wakati wa mbunguo nyuklia unatokea hasa kwa namna tatu zinazotajwa kwa herufi za Kigiriki alfa, beta na gamma kuwa mnururisho α, mnururisho β na mnururisho γ. Kati ya hizi kila moja inaweza kuwa hatari kwa binadamu na viumbehai kutegemeana na kiwango chake lakini hatuna mlango wa fahamu wa kuitambua.


Marejeo

Tovuti za Nje