Luka Jović

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Luka Jović (amezaliwa 23 Desemba 1997) ni mchezaji wa soka wa Serbia ambaye anacheza katika klabu ya Hispania Real Madrid na timu ya taifa ya Serbia kama mshambuliaji.

Jovic mwenye jezi nambari 19.

Jović alizaliwa katika kijiji kidogo cha Batar Serbia. Katika umri wa miaka mitano, alianza kucheza mpira huko Loznica. Jović alipewa nafasi ya kucheza katika klabu ya Red Star Belgrade mnamo 2005. Kabla ya kufanya hivyo, baba yake alimtaka afanye mazoezi na Partizan, ambaye alikuwa akijaribu kumsainisha Jović kwa muda mrefu na kushindikana. Mnamo Februari 2016, Jović alisaini na mabingwa wa Ureno Benfica hadi 2021.

Mkataba wa Jovic kukaa Benfica mpaka 2021 ulivunjwa na kusainiwa na Real Madrid kwa ada ya milioni 60 mpaka mwaka 2025.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luka Jović kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.