Nenda kwa yaliyomo

Lugha za Kihindi-Kiirani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lugha za Kihindi-Kiulaya; buluu: maeneo ya lugha za Kihindi-Kiirani

Lugha za Kihindi-Kiirani ni kundi kubwa zaidi katika familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Zinajumuisha lugha za Kihindi-Kiarya na lugha za Kiirani (Irani). Zinazungumzwa zaidi kwenye Bara Hindi na Nyanda za Juu za Iran. Hapo zamani zilitumiwa pia katika Asia ya Kati, mashariki mwa Bahari ya Kaspi .

Lugha za Kihindi-Kiarya

[hariri | hariri chanzo]

Kuna karibu lugha 221 za Kihindi-Kiarya (Kiing. Indic), zenye jumla ya wasemaji zaidi ya milioni 800.

Lugha za Kiirani (Kiajemi)

[hariri | hariri chanzo]

Kuna karibu lugha 86 za Kiirani, zenye wasemaji kati ya milioni 150 hadi 200.

Kinuristani, Kibangani, na Kibadeshi

[hariri | hariri chanzo]

Wasomi wengine huchukulia lugha za Kinuristani na Kibangani kama sehemu ya kikundi kidogo cha Kihindi-Kiarya, lakini wengine wanazichukulia kama vikundi viwili tofauti vya Kihindi-Kiirani. Lugha ya Kibadeshi pia ni lugha ya Kihindi-Kiirani isiyopangwa bado kimakundi.

  • Cardona, George. Indo-Iranian languages. Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2018.{{cite encyclopedia}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Indo-Iranian. Ethnologue. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2018.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: others (link)