Krioli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lugha ya krioli)
Bango barabarani likitumia krioli ya Guadeloupe.

Krioli (kwa Kiingereza: creole language) ni jina la kutaja lugha yoyote[1][2][3] iliyokua kutokana na lugha mbili au zaidi kukutana na kuingiliana. Hivyo inatokana na matumizi ya pijini kwa muda mrefu, yaani ni pijini iliyokua na kupata wasemaji wake asilia. Hivyo basi hapawezi kuwa na krioli pasipokuwa na pijini kwanza.

Kuna lugha za Krioli nyingi duniani. Lugha hizo huwa na miundo changamano. Pia zina msamiati mwingi kutoka lugha mbalimbali, jambo linaloitofautisha pakubwa na lugha asilia.

Idadi ya lugha za aina hiyo ni walau 100, na nyingi kati yake zimetokana na lugha za Ulaya.

Krioli kubwa zaidi ni ile ya Haiti, yenye wasemaji zaidi ya milioni 10[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krioli kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.