Lucilla Boari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lucilla Boari (alizaliwa Mantova, 24 Machi 1997) ni Mwitalia mpiga mishale ambaye aliiwakilisha Italia mwaka 2016 katika mashindano ya olimpiki ya majira ya joto na mwisho wa mwaka 2020. Pia aliweza kushindana kwa ajili ya nchi yake mwaka 2018 kwenye michezo ya Mediteranea na mwaka 2019 kwenye michezo ya ulaya, ambapo alishinda medali za mmoja mmoja, medali ya dhahabu na ya fedha moja baada ya nyingine.

Maisha ya kazi[hariri | hariri chanzo]

2016 Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto[hariri | hariri chanzo]

Boari aliiwezesha nchi yake kufuzu kwenye michezo iliyokuwa ni mashindano ya dunia ya majira joto ya olimpiki 2016, kupelekea malalamiko kutoka Taipei ya china baada ya italia kupewa ushindi wote wa mashindano ya olimpiki kwa wapiga mishale watatu dhidi yao. . Boari baadae alichaguliwa kuwa kwenye kikosi cha italia pamoja na watangulizi wenzake wa olimpiki Claudia Mandia na Guendalina SartoriJulai 2016[1].

20182019: Baada ya Michezo ya Olimpiki[hariri | hariri chanzo]

Juni 2018 Boari alishinda medali ya dhahabu kwenye matukio ya wanawake ya mmoja mmoja michezo ya mediterania, akimshinda muhispania Mónica Galisteo Cruz kwenye fainali[2].

2020 Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2021 alishinda medali ya shaba kwenye mashindano ya olimpiki yaliyofanyika 2020 majira ya joto kwenye matukio ya wanawake mmoja mmoja[3]. Kipindi hicho pia alijihusisha na mahusiano ya jinsia moja, akifichua kwamba mholanzi mpiga mishale Sanne de Laat ni mpenzi wake wa jinsia ya kike[4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maitre Wicki, Ludivine (7 July 2016). "Archery Italy displays Olympic and Paralympic teams for Rio". World Archery Federation. Iliwekwa mnamo 1 September 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Turkish teenager tastes archery success at Tarragona 2018 Mediterranean Games". www.insidethegames.biz. 1529853540. Iliwekwa mnamo 2021-11-29.  Check date values in: |date= (help)
  3. "Lucilla BOARI". Olympics.com. Iliwekwa mnamo 2021-11-29. 
  4. Flavio Vanetti (2021-07-30). "Lucilla Boari alle Olimpiadi, chi è il bronzo storico nel tiro con l’arco (e quella vecchia polemica sulle “cicciottelle”)". Corriere della Sera (kwa it-IT). Iliwekwa mnamo 2021-11-29.