Louis Simpson
Mandhari
Louis Aston Marantz Simpson (27 Machi 1923 – 14 Septemba 2012) alikuwa mshairi kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa nchini Jamaika, babake akiwa na mababu kutoka Afrika na Uskoti, mamake akiwa Myahudi kutoka Urusi. Simpson akiwa na umri wa miaka 17 tu akahamia Marekani kusomea lugha ya Kiingereza chini ya Profesa Mark Van Doren. Baada ya Marekani kuingia Vita Kuu ya Pili ya Dunia Simpson akawa mwanajeshi na miaka ya 1943-1945 akafanya kazi ya kijeshi nchini Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji na Ujerumani. Alitunga mashairi kuhusu uzoefu wake wa vita. Mwaka wa 1964 alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Louis Simpson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |