Louis Nganga a Ndzando
Mandhari
Louis Nganga a Ndzando (1923 – 13 Februari 2014) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ndzando alizaliwa Ndeke Mabela na alitunukiwa daraja ya upadre mnamo 23 Februari 1953. Aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Lisala, na pia askofu wa Jimbojina la Athyra, mnamo 18 Aprili 1961 na alipewa daraja ya uaskofu mnamo 9 Julai 1961.
Ndzando aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la Lisala mnamo 25 Novemba 1964 na alistaafu kutoka jimbo hilo mnamo 6 Julai 1997.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |