Lorna Laboso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lorna Laboso

Lorna Chepkemoi Laboso (8 Novemba 1961 - 10 Juni 2008) alikuwa mwanasiasa wa Kenya na mwanachama wa Orange Democratic Movement (ODM).

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Laboso alipata alipata shahada ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Daystar mnamo 2007.

Ubunge[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa Mbunge wa Sotik kwa kipindi kidogo baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 2007. pia aliwahi kuhudumu kama naibu wa Waziri mnamo 2008. [1] Ilikuwa mara yake ya kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa 2007 kama mbunge wa Sotik.[2] Katika serikali ya Muungano ya 2008, alichguliwa kuwa Naibu wa waziri katika Ofisi ya Makamo wa Rais.[1]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Aliuawa pamoja na Waziri wa barabara Kipkalya Kones kwenye ajali ya Ndege mnamo 10 Juni 2008.[3] [4] Ndege hiyo iligonga nyumba katika soko la Kajong'a karibu na Nairagie Enkare, pale Enoosupukia, Wilaya ya Narok,[1] karibu na Narok[3][4] na Mbuga ya wanyama ya Masai Mara[4] Ndege iliyokuwa ikiwabeba ilikuwa imeondoka Uwanja wa Ndege wa Wilson mjini Nairobi; [1] [3] [4] walikuwa wakielekea Kericho katika kampeni za mgombea wa ODM katika uchaguzi mdogo wa Ainamoi mnamo 11 Juni,2008.[1]. Pia rubani wa ndege hiyo na mlinda Usalama walifariki.[1][4] Rais Mwai Kibaki alituma risala za rambirambi na kuamrisha kupeperushwa kwa bendera Nusu Mlingoti. Waziri Mkuu Raila Odinga ambaye ni Kinara wa ODM alisema pia kuwa ilikuwa hali ya huzuni sana.[1]

Kuhusu Vurugu ya baada ya Uchaguzi wa 2007[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya washukiwa waanzilishi wa mchafuko uliotokea baada ya uchaguzi wa 2007 inataja jina lake kama mmoja wa washukiwa wa nafasi ya kwanza (uk. 177) na anashtakiwa kwa"Kupanga vita na kuchochea". Kiini: www.knchr.org Archived 29 Julai 2009 at the Wayback Machine.

Uchaguzi Mdogo[hariri | hariri chanzo]

Kufuatia kifo cha Laboso, uchaguzi mdogo ulifanyika katika Eneo Bunge la Sotik mnamo 25 Septemba 2008. Uchaguzi huo ulishindwa na dadake Laboso, Joyce Cherono kwa tikiti ya ODM.[5]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Joyce Cherono Kipkalya Kones

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Dominic Wabala and Fred Mukinda, "Kones killed in crash" Archived 13 Juni 2008 at the Wayback Machine., Daily Nation, 11 Juni 2008.
  2. "Kenya Mourns its legislators: Kipkalya Kones and Lorna Laboso die in a Plane Crash." Archived 17 Agosti 2021 at the Wayback Machine., Kenya London News.
  3. 3.0 3.1 3.2 "Two Kenyan government ministers die", Sapa-AFP (IOL), 10 Juni 2008.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 "Ministers killed in Kenya crash", BBC News, 10 Juni 2008.
  5. The Standard, 26 Septemba 2008: ODM Yashinda katika Bomet na Sotik Archived 10 Desemba 2009 at the Wayback Machine.