Liri Gero
Liri Gero (1926–1944) alikuwa mwanaharakati kijana wa kikomunisti wa Albania na mwanachama wa vuguvugu la upinzani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Akipigana pamoja na majeshi ya wanamgambo (partisans), aliuawa katika mapambano dhidi ya Wanazi. Kwa ushujaa wake, alitunukiwa tuzo ya Shujaa wa Watu wa Albania.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Gero alikuwa Mwalbania mwenye asili ya Waaromani,[1] alizaliwa mjini Fier, katikati mwa Albania, mnamo mwaka wa 1926. Akiwa bado mdogo sana, alijihusisha na vuguvugu la upinzani kama sehemu ya vikundi vya kikomunisti vilivyopinga Uvamizi wa Italia nchini Albania na uvamizi wa Kifashisti. Nyumba yao ilikuwa moja ya "nyumba salama" zilizotumiwa na wanachama wa upinzani kwa ajili ya shughuli zao. Mnamo tarehe 14 Septemba 1943, Gero na wasichana wengine 67 kutoka Fier, na kufanya jumla yao kuwa 68, walijiunga usiku huo huo na safu ya wanamgambo wa Vuguvugu la Ukombozi wa Kitaifa tukio hili lilikuwa la kihistoria na la kukumbukwa katika harakati za upinzani za Albania, ikizingatiwa kuwa mji wa Fier ulikuwa na wakazi wapatao 5,000 tu wakati huo.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Vllehtë në hapësirat myzeqare". Gazeta Dita (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-20. Iliwekwa mnamo 2021-12-29.
- ↑ Nasho Jorgaqi (2014-09-14), 68 vajza fierake dolën partizane në një ditë [68 girls from Fier joined the ranks of the partisans on the same day] (kwa Albanian), Gazeta Dita, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-27, iliwekwa mnamo 2015-12-21
{{citation}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liri Gero kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |