Nenda kwa yaliyomo

Linda Fagan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Admiral_Linda_L._Fagan,_Coast_Guard_Vice_Commandant
Linda Fagan,2021.

Linda Lee Fagan (amezaliwa Julai 1, 1963[1][2]) ni admirali mstaafu wa jeshi la majini la Marekani ambaye alihudumu nafasi ya kamanda mkuu wa 27 katika jeshi la ulinzi wa pwani la Marekani kuanzia Juni 2022 hadi Januari 2025[3]. Hapo awali alikuwa kamanda msaidizi wa jeshi la ulinzi wa pwani chini ya Kamanda Karl L. Schultz kuanzia 2021 hadi 2022.[4]

Kabla ya hapo alikuwa kamanda katika eneo la Pasifiki,akihudumu katika jeshi la ulinzi wa pwani, na pia aliwahi kuwa msaidizi wa Walinzi wa Pwani anayeshughulikia Operesheni,Sera na Uwezo,vile vile alihudumu kama kamanda wa wilaya ya kwanza ya walinzi wa pwani na kamanda wa sekta ya walinzi wa pwani wa New York. Mnamo Aprili 2021,aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani,bwana Alejandro Mayorkas alitangaza uteuzi wake kuwa kamanda msaidizi wa jeshi la ulinzi wa Pwani, kuchukua nafasi ya Charles W. Ray.[5]

Tarehe 17 Juni 2021,Fagan alithibitishwa na kuanza rasmi kazi yake tarehe 18 Juni.[6] Mnamo Aprili 2022 ilitangazwa kuwa Fagan amependekezwa kumrithi Schultz kama kamanda wa jeshi la ulinzi wa Pwani, jambo ambalo lilimfanya kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuongoza tawi la jeshi la Marekani.[7]

Uteuzi wake ulipelekwa kwa Seneti ya Marekani tarehe 7 Aprili 2022 na kuthibitishwa kwa ridhaa ya pamoja tarehe 11 Mei.[8] Alianza rasmi kushika wadhifa huo tarehe 1 Juni.[9]

Tarehe 21 Januari 2025, Fagan alivuliwa madaraka,baada ya kuapishwa kwa Rais Donald Trump,[10] jambo lililomfanya pia kuwa kamanda wa kwanza kuondolewa madarakani.[11]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika jiji la Columbus, Ohio.Baadaye,alihitimu katika chuo cha mafunzo ya kijeshi,ambacho kipo chini ya jeshi la ulinzi wa pwani la Marekani mwaka 1985 akiwa na shahada ya kwanza katika sayansi ya bahari. Baadaye alipata shahada ya uzamili ya masuala ya baharini kutoka chuo kikuu cha University of Washington mwaka 2000 na shahada ya uzamili katika mkakati wa usalama wa taifa kutoka katika Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa mwaka 2008.

Ushughulikiaji wa uchunguzi wa unyanyasaji wa kingono

[hariri | hariri chanzo]

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya Fagan kuwa kamanda, katikati ya mwaka 2023 ilifichuliwa kuwa maafisa wa jeshi la ulinzi wa Pwani, walifanya uchunguzi kati ya 2014–2018 kuhusu visa vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika Chuo cha jeshi la ulinzi wa Pwani, lakini hawakuwafahamisha bunge kuhusu uchunguzi huo.

Fagan aliomba msamaha kwa waathiriwa wa unyanyasaji huo na kuahidi kuwa wazi zaidi kuhusu matatizo ndani ya taasisi hiyo.[12] Baada ya kusikiliza ushuhuda wa wanawake wanne waliodaiwa kubakwa, wanachama wa kamati ndogo ya kudumu ya uchunguzi ya seneti ,waliapa kuwawajibisha viongozi wa zamani na wa sasa wa jeshi la ulinzi wa Pwani.

Seneta wa jimbo la Connecticut,bwana Richard Blumenthal,ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ndogo, alisema watawafuatilia watu waliotajwa akiwemo admirali mstaafu Karl L. Schultz pamoja na Fagan.

Mnamo Desemba 19, 2023 kamati hiyo ilisema kuwa utamaduni wa kuficha matukio ndani ya jeshi la ulinzi wa Pwani,umeruhusu unyanyasaji wa kingono kuendelea kwa miongo kadhaa katika chuo hicho na ndani ya taasisi yenyewe.

Kuondolewa madarakani

[hariri | hariri chanzo]

Fagan alivuliwa madaraka tarehe 21 Januari 2025 na naibu Waziri wa Usalama wa Ndani, Benjamine Huffman. Wakati huo alikuwa bado na miaka miwili iliyobaki katika muhula wake wa miaka minne.[13] Taarifa kutoka kwa afisa mwandamizi wa Wizara ya Usalama wa Ndani ilisema kuondolewa kwake kulihusishwa na:

• kushindwa kushughulikia vitisho vya usalama mpakani

• uongozi dhaifu katika ajira na uhifadhi wa wanajeshi

• usimamizi mbaya wa miradi muhimu kama meli za kuvunja barafu na helikopta

• kuzingatia sana mipango ya utofauti, usawa na ujumuishaji

• kupungua kwa imani kutokana na kushughulikia vibaya Operesheni ya nanga .

Mbunge Rick Larsen alikosoa uamuzi huo akisema ni wa kupotosha na unaweza kudhoofisha utayari wa Walinzi wa Pwani. Seneta Maria Cantwell pia alipinga uamuzi huo akisema kufukuzwa kwa kamanda na rais mpya kunaweka mfano mbaya kwa taasisi hiyo.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, Fagan alipata habari za kufukuzwa kwake wakati wa hafla ya sherehe ya kijeshi katika siku ya kuapishwa kwa rais mpya.

Pia iliripotiwa kuwa alitolewa kwenye makazi yake tarehe 4 Februari akiwa amepewa taarifa ya saa tatu tu.

Maisha binafsi na familia

[hariri | hariri chanzo]

Fagan alizaliwa na Jon Harley Keene na mkewe Loann Carol (Morris) Keene.[14]

Ana mabinti wawili, mmoja wao ni mhitimu wa Chuo cha jeshi cha ulinzi wa Pwani.[15]

  1. "Biographical Information and Qualifications of Linda L. Fagan". U.S. Senate Committee on Commerce, Science and Transportation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 20, 2021. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Senate Commerce Committee Coast Guard Nominee Questionnaire, 117th Congress - Linda L. Fagan". U.S. Senate Committee on Commerce, Science and Transportation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 26, 2021. Iliwekwa mnamo 2021-05-13.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Admiral Linda L. Fagan". United States Coast Guard. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2026.
  4. "Adm. Linda Fagan Becomes USCG's First Female Four-Star Admiral". The Maritime Executive. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 3, 2021. Iliwekwa mnamo Juni 2, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Vice Admiral Linda L. Fagan". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 25, 2021. Iliwekwa mnamo 2021-04-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "U.S. Coast Guard welcomes new vice commandant". U.S. Coast Guard. 2021-06-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Novemba 15, 2022. Iliwekwa mnamo 2021-06-19.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. LaGrone, Sam (2022-04-05). "Biden Nominates Adm. Linda Fagan to Head Coast Guard, First Woman to Lead Military Service". USNI News. National Harbor, Maryland. Iliwekwa mnamo Aprili 5, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "PN1947 — Adm. Linda L. Fagan — Coast Guard, 117th Congress (2021-2022)". 2022-04-07.
  9. "Fagan to be first woman to serve as Coast Guard commandant". 2022-04-12.
  10. Johnson-Freese, Joan, Firing of Coast Guard commandant serves a regressive social agenda, Florida Phoenix, January 25, 2025
  11. Mongilio, Heather (2025-01-21). "Updated: Adm. Linda Fagan Removed as Coast Guard Commandant". {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  12. "Former Coast Guard head covered up secret investigation into sexual assaults at the Coast Guard Academy".
  13. "Trump administration fires Coast Guard Commandant Linda Fagan". {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  14. "Certificate of Birth". Birth Records. Na. 106567. Columbus, Ohio: Ohio Vital Records Office. 1963.
  15. https://www.commerce.senate.gov/2022/4/nomination-hearing-for-u-s-coast-guard-commandant-nominee-admiral-linda-fagan. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)