Nenda kwa yaliyomo

Linda-Gail Bekker

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Linda-Gail Bekker MBChB, DTMH, DCH, FCP(SA) ni profesa wa Tiba na Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu . Pamoja na hayo ni Mkurugenzi wa Kituo cha VVU cha Desmond Tutu ndani ya Chuo Kikuu cha Cape Town. Yeye ni Rais wa Zamani wa Jumuiya ya Kimataifa ya UKIMWI (2016–18). [1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Bekker alizaliwa nchini Zimbabwe. [2] Alipata masomo yake ya udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Cape Town. [3] Alilenga hapo awali kuwa daktari wa wazee, lakini maamuzi hayo yalibadilika baada ya mzunguko wa kliniki huko KwaZulu-Natal na akapendezwa zaidi na utafiti wa VVU na Kifua Kikuu. [4] Aliwaona vijana wakifariki kutokana na VVU/UKIMWI na aliumia kwamba hakuweza kuwasaidia. [5] Shahada yake ya Uzamivu (PhD) ilifadhiliwa na Kituo cha Kimataifa cha John E. Fogarty . [2] Alifanya kazi ndani ya Chuo Kikuu cha Rockefeller juu ya kinga mwilini. [2] Mshauri wake wa udaktari alikuwa Gilla Kaplan na anaendelea kufanya kazi naye hadi leo. [6] [5]

Utafiti na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2009 alishinda Tuzo ya Royal Society Pfizer kwa utafiti wake juu ya magonjwa ya kifua kikuu . [7] Ufadhili huo uliipa nguvu utafiti wake kwenye Kliniki ya Afya ya Msingi ya Nyanga mahali panaitwa Cape Town. [7] Bekker ana shauku ya kushirikiana na jamii na programu za elimu zinazoongozwa na rika. [8] Kazi yake ya kijamii inalenga kushinda unyanyapaa unaohusiana na VVU na Kifua Kikuu . [9] Wakfu wa Desmond Tutu HIV, ambapo Bekker anashikilia nafasi ya Afisa Mkuu wa Uendeshaji, husaidia ustawi wa watu kwenye jamii maskini zaidi ndani ya Afrika Kusini. [10] Mume wake, Robin Wood, anatumika kama Mkurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji. Alitengeneza gari la afya linaloweza kuhamishika, linalojulikana kama kipimo cha Tutu, ambalo hutoa uchunguzi wa ujauzito, shinikizo la damu, kisukari, VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na unene kupita kiasi. [11] [9] Yeye ni Mkurugenzi wa Kituo cha VVU cha Desmund Tutu katika Chuo Kikuu cha Cape Town, ambapo anajumuisha taarifa bora na zenye ushahidi juu ya matibabu na kinga ya vijana kwenye jukwaa thabiti. Kituo hicho kinafadhiliwa na Taasisi za Kitaifa za Afya . Alitengeneza Chaguo za Mbinu za Kinga za Vijana Afrika Kusini (CHAMPS); ambacho kinaenda kinyume na mitazamo ya vijana wa kiume kuhusu tohara, kinawahimiza wanawake vijana kutumia njia za uzazi wa mpango na kuchunguza kinga dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI (AWAMU) zinazofadhiliwa na Taasisi za Kitaifa za Afya . [12] uanzishaji wa tiba za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi . [13] [14] Anafurahi kuhusu kujipima VVU.

Mwaka wa 2016 alichaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya ya Kimataifa ya UKIMWI . Alisoma hotuba ya ufunguzi Kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Jumuiya ya UKIMWI huko mjini Paris, ambapo alielezea kuhusu njia mpya za kinga kama vile kinga ya kabla ya kuambukizwa . Mwaka wa 2018 alichaguliwa kuwa mwanachama wa bodi ya Mpango wa Kimataifa wa Chanjo ya UKIMWI . Ana wasiwasi kuhusu Donald Trump kudhoofisha mwitikio wa kimataifa wa VVU. [15] Amekuwa mzungumzaji mkuu kwenye Siku ya UKIMWI Duniani . [16]

Amechangia mawazo yake kwenda The Conversation . Bekker anapendelea uchoraji na ametumia njia za sanaa za mitaani katika kazi zake za kijamii. [9]

Bekker ameshikilia nafasi ya mshauri wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupunguza UKIMWI .

Ndani ya Mkutano wa Kimataifa wa UKIMWI wa mwaka wa 2024 huko Munich, Profesa Bekker aliwasilisha majibu kutoka kwa utafiti wa PURPOSE-1 wa kuzuia VVU kwa kutumia lenacapavir inayodungwa mara mbili kwa mwaka ambayo ilionyesha kuwa sindano ya mara mbili kwa mwaka inalinda kikamilifu wanawake kutokana na maambukizi ya VVU. [17] Hakuna washiriki waliopokea maambukizi ya VVU ya lenacapavir iliyopatikana mara mbili kwa mwaka pia iliripotiwa katika makala ya The New England Journal of Medicine . [18]

UVIKO-19

[hariri | hariri chanzo]

Bekker alikuwa mchunguzi mwenza mkuu, wakishirikiana na Glenda Gray, wa jaribio la Sisonke lililolenga kuwapa wafanyakazi wa afya nchini Afrika Kusini ufikiaji wa mapema wa chanjo za COVID. [19] Jaribio la kliniki la awamu ya 3b lililokua linafanya kazi lilianza kwenye tarehe ya 17 Februari 2021 [20] hadi tarehe ya 15 Mei 2021, [21] huku dozi 478,733 zikitolewa kwa wafanyakazi wa afya. [22] Utafiti huo ulijaribu uimara wa chanjo ya Jansen (J&J) inapotolewa kwa kiwango kikubwa chini ndani ya mazingira Afrika Kusini. [19]

  1. Samarasekera, Udani (2021). "Linda-Gail Bekker—a leader at the service of the world". The Lancet Infectious Diseases. 21 (6). Elsevier BV: 778. doi:10.1016/s1473-3099(21)00283-8. ISSN 1473-3099. PMID 34051192. S2CID 235248719.
  2. 1 2 3 "Q and A with former Fogarty trainee Dr Linda-Gail Bekker". FIc (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  3. "The NS Interview: Linda-Gail Bekker". www.newstatesman.com (kwa Kiingereza). 5 Novemba 2009. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Vax Report - Vax Report". www.vaxreport.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  5. 1 2 "PHRI :: Gilla Kaplan, Ph.D." www.phri.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Juni 2003. Iliwekwa mnamo 14 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Gilla Kaplan". Bill & Melinda Gates Foundation (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2013. Iliwekwa mnamo 14 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 1 2 "African scientist wins award for HIV and TB co-infection research - Science News". royalsociety.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  8. "Professor Linda-Gail Bekker MBChB DTMH DCH FCP(SA) PhD | Infectious Disease & Molecular Medicine". www.idm.uct.ac.za (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-29. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  9. 1 2 3 "Linda-Gail Bekker: confronting the TB/HIV co-infection epidemic" (PDF). The Lancet. 2013-02-13. Iliwekwa mnamo 2018-05-28. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name ":3" defined multiple times with different content.
  10. "Linda-Gail Bekker". The Conversation (kwa Kiingereza). 21 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "FABA (For Africa By Africans: Tutu Tester | Africa Strictly Business". www.africastrictlybusiness.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-29. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  12. "Team". PHASES: Pregnancy & HIV/AIDS: Seeking Equitable Study (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  13. "Conference Committees". www.aids2018.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  14. Bekker, L.-G.; Wood, R. (2011-11-01). "TB and HIV co-infection: When to start antiretroviral therapy". Continuing Medical Education (kwa Kiingereza). 29 (10): 420. ISSN 2078-5143. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2018.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Cutbacks in foreign aid for HIV treatment would produce great harm, generate few savings". Massachusetts General Hospital (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 14 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. Expresso Show (2017-12-04), World Aids Day – Linda-Gail Bekker, iliwekwa mnamo 2018-05-28
  17. Sax, Paul (2024-07-25). "Lenacapavir PrEP Trial Brings Down the House at the International AIDS Conference". HIV and ID Observations (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-07-27.
  18. Bekker, Linda-Gail; Das, Moupali; Abdool Karim, Quarraisha; Ahmed, Khatija; Batting, Joanne; Brumskine, William; Gill, Katherine; Harkoo, Ishana; Jaggernath, Manjeetha; Kigozi, Godfrey; Kiwanuka, Noah; Kotze, Philip; Lebina, Limakatso; Louw, Cheryl E.; Malahleha, Moelo (2024-07-24). "Twice-Yearly Lenacapavir or Daily F/TAF for HIV Prevention in Cisgender Women". New England Journal of Medicine (kwa Kiingereza). 391 (13): 1179–1192. doi:10.1056/NEJMoa2407001. ISSN 0028-4793. PMID 39046157.
  19. 1 2 Patel, Khadija (16 Machi 2021). "Trials, tinsel & tango: Go inside Linda-Gail Bekker's COVID world – Bhekisisa". Bhekisisa. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  20. "J&J vaccines arrive in SA on Tuesday night". TimesLIVE. 16 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. Nair, Nivashni (15 Mei 2021). "Final vaccine administered as part of Sisonke trial". TimesLIVE. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. "Update On Covid-19 (16th May 2021)". SA Corona Virus Online Portal. 16 Mei 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)