Nenda kwa yaliyomo

Limau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Limao)
Limau nzima na limau nusu.
Limau bivu na ua lake.

Limau (pia: limao; kutoka Kiarabu ليمون limun) ni tunda la mlimau, mti mdogo ambao daima kijani, Citrus limon, asili yake ni Asia. Pamoja na chungwa, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa.

Rangi ya tunda lililoiva ni njano hadi njano-kijani. Majimaji yake yana asidi nyingi: ni asilimia 5 asidi sitriki (asidi maalumu ya matunda jamii ya machungwa) ambayo hulipa limao ladha yake ya uchachu, na ph ya 2 mpaka 3, kiasi kwamba tunda haliliwi moja kwa moja kutokana na uchungu mkali.

Matumizi yake ni katika upishi hasa: nyama yake na pia maganda yake hutumika hasa wakati wa kupika na kuoka. Kutokana na ladha yake ya uchachu, vinywaji vingi na peremende vilivyokolezwa na ladha ya limao vinapatikana. Majimaji yake hutumiwa kwa ajili ya vinywaji ama kama kiungo pamoja na maji ya matunda mengine au mara nyingi kwa kuongeza sukari na maji.

Mengine yasiyo ya mapishi hasa ni majimaji yake ambayo hufanya kujipatia asidi ya gharama nafuu kwa ajili ya mafunzo ya kielimu.

Limau ina vitamini C nyingi ndani yake na kiasi kidogo kinatosheleza mahitaji ya binadamu. Sifa hii ilitambuliwa wakati mabaharia kwenye jahazi walipata ugonjwa wa kiseyeseye uliokuwa balaa kwa safari za kwanza zilizovuka bahari za Atlantiki na Pasifiki wakati wa upanuzi wa Wareno, Wahispania na Waingereza kuanzia karne ya 16. Hapo limau zilitambuliwa kuwa dawa iliyozuia ugonjwa huo kutokana na kiasi chake cha vitamini C.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Asili kabisa ya limao bado haijulikani, japo inaaminika kuwa mimea ya kwanza ilipatikana huko India, Kaskazini mwa Bama na China. Huko Kusini na kusini Mwashariki mwa asia yalifahamika kwa uwezo wake wa matibabu na ukatumika sana kama dawa kwa sumu mbalimbali. Baadae ukafahamika huko Persie na kasha Misri na Iraki mnamo 700bk. Mlimao ulisambaa sana miongoni mwa jamii ya Uarabu na Ukanda wa Mediteraniani kati ya 1000 na 1150 BK. Malimao yaliingia ulaya baada ya karne ya kwanza BK, wakati wa utawala wa Roma.

Nchini Moroko malimau hupikwa na chumvi yakikaa kwa muda kuiva; hutumiwa kama kiungo cha upishi

Hata hiyo mmea huuulikua hauliwi sana na kilimo cha limao kilianza karne ya kumi na tano huko Genoa. Baada yalifika mpaka mpaka America mwaka 1493 wakati ambapo Cliristopher Columbus alichukua mbegu za limao na kwenda nazo Hispania wakati wa safari zake. Kutoka Hispania malimao yalisambaa sana na yalikuwa yakitumika hasa kwa mapambo na dawa na miaka ya 1700 na 1800, malimao yalikuzwa sana huko Fhorida na Calfonia baada ya malimao kuanza kutumika kupikia na kama viungo vya kuongeza laza. Mnamo 1747 utafiti wa James Lind ulithibitisha kwamba unavitamini C kutoka kwenye limao, yaliweza kuwatibu baharia ugonjwa wa ngozi wa kiseyeye.

Virutubisho vya limao

[hariri | hariri chanzo]

Malimao yanafahamika kama msaada mkubwa wa umengenywaji wa chakula, mchanganyiko wa asali nyeusi na makapi huwa kwa kiwango kizuri katika kusafisha oganiza umegaji wa chakula. Virutubisho vingine hujumuisha maji -89%, aside ya sitriki -5%, makapi -2.8%, sukari – 2.5%, mafuta – pungufu ya 0.3%, protini – pungufuya 7%, vitamin C, na madini kadhaa kama vile selenium, zinc manganese, na shaba. Vitamin C katikt limao hutofautina. Hutegemea na ukubwa na ukomavu, kuiva aina na sehem inayoliwa kula limao lililokomaa huwezesha mtu kupata 10,000% ya vitamin c. Zingatia kuwa ni lile ganda la ndani jeupe la ndani la limao, linalokuwa na kiasi kikubwa cha vitamin c kwa ujazo wake kuliko chakula kingine chochote, uchunguzi unaonyesha, sehem ile nyeupe kuwa na mara 8 mpaka 11 zaidi ya vitamin c kuliko chupa ya dawa ya vitamin c kutoka hospitali.

Matumizi katika mapishi

[hariri | hariri chanzo]

Malimao hutumika kutengenezea shamlati na mapambo mezani kwa vinywaji. Magada ya limao pia yanamatumizi mengi. Vinywaji vingi soda, chi na maji mara nyingi huandaliwa na kipande cha limao kwenye bilauri au hata kwenye pindo ya chombo husika. Ssamaki huwekwa maji ya limao kuondoa shombo. Hapo aside ya limao hubadilisha amaibni, kemikali iliyo kwenye samaki kuwa chumvi za amoniamu, pia hutumika kulainisha nyama kwa tena kunyunyizia kwenye nyama kabla ya kupika, japo haiui vijidudu. Mmatumizi mengine, malimao hutumika kutengeneza aside ya Sitriki, kabla ya njia ya kuchachusha haijafahamika. Hutumika kusafishia vyombo na baadhi ya vitu hasa, hasa kwa ugumu wake ya kuondoa mafutana madoa.Hutumika kama bacteria sababu ya kiwango chake kidogo cha pH, majimaji ya limao pia hutumika kusafishia vyombo vya shombo, wakifuatiwa na Meksiko 14.5%, Brazili 8% na Hispania 7%.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Limau kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.