Lilly Platt
Lilly Platt (amezaliwa 18 Aprili 2008) ni mwanamazingira Mholanzi aliyezaliwa Uingereza. Platt anajulikana kwa udogo wa umri katika kufanya mgomo wa amani inayolenga kutoa sauti juu ya masuala ya uharibifu wa mazingira.[1] Yeye ni balozi wa kimataifa wa YouthMundus,[2] Earth.org,[3] na WODI;[4] balozi wa vijana wa muungano wa uchafuzi wa plastiki na How Global;[5] na balozi mtoto wa siku ya Usafi Duniani.[6] Awali Platt alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurusha picha za takataka za plastiki alizookota na kuzipanga ipasavyo. Kwa miaka mingi ameokota zaidi ya vipande 100,000 vya takataka.[7]
Platt alizaliwa Uingereza.[8] Familia yake ilihamia Uholanzi alipokuwa na umri wa miaka saba.
Utuzaji wa Mazingira
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka wa 2015, Platt alivyokuwa akitembea kando ya bustani huko Uholanzi na babu yake aliona takataka za plastiki zimetawanyika chini. Aliamua kuzihesabu ili kufanya mazoezi yake ya lugha ya Kiholanzi. Walikusanya vipande 91 vya plastiki ndani ya dakika 10.[7] Babu yake alimweeleza zaidi jinsi takataka zinavyoishia kuwa supu ya plastiki.[9] Tukio hilo ndio liliyosemekana kama lilianzisha mpango wake wa mazingira, na akiwa na umri wa miaka 7, alianza Lilly's Plastic Pickup. Kupitia Lilly's Plastic Pickup , yeye huchukua taka na kuzipanga kwa uangalifu. Aliziweka kwenye mitandao ya kijamii ili kuongeza ufahamu kuhusu suala hilo.[7] Kwa miaka mingi Platt ameokota zaidi ya vipande 100,000 vya taka, kuanzia chupa, vifuko vya sigara, katoni za vinywaji n.k. Kupitia Lilly's Plastic Cleanup, Platt pia anashiriki athari za plastiki kwa wanyamapori na mfumo ikolojia.[10] Tokea kupata umaarufu kwa kasi mradi wake umepata sifa ya kimataifa.[7]
Tangu alipokuwa mtoto, Platt alionyesha upendo kwa wanyama, hasa wale wanaoonekana kuwa wasiovutia. Alionewa shuleni kwa sababu ya hili, na ni mmoja tu kati wenzake wa rika lake aliyeonyesha kupendezwa na shughuli zake za usafishaji. Kisha Platt alihamia The King's School ambapo wanafunzi wenzake wengi walishiriki katika jitihada zake za kusafisha mazingira.[1]
Katika uchaguzi wa Uholanzi wa mwaka 2019, babu yake na Platt alipiga kura kwa niaba yake, alipokuwa akifanya kampeni ya kupiga marufuku plastiki. Platt alichukua video na kuwatia moyo wengine kufanya vivyo hivyo.[7]
Mnamo septemba mwaka 2018, Platt aliona maandamano ya Greta Thunberg nje ya bunge la Uswidi kuhusu utekelezaji wa Makubaliano ya Paris. Alitiwa moyo na kuamua kugoma. Baada ya wiki chache, Greta Thunberg alijiunga na mgomo wa Platt nchini Uholanzi, ikizingatiwa Uholanzi ilikuwa mojawapo ya watoaji wa juu zaidi wa gesi chafu katika Umoja wa Ulaya. Wote wawili walialikwa Brussels ambako walihudhuria mkutano wa hali ya hewa nje ya Bunge la Ulaya.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 "This Plastic Pickup Extraordinaire Will Always Have Your Back: Meet Lilly Platt", Climate Kids (kwa American English), 2019-01-04, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-14, iliwekwa mnamo 2025-10-07
- ↑ YouthMundus (2019-04-29). "Meet 11 Year Old Lilly - YouthMundus' Global Youth Ambassador". YouthMundus Festival (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ Earth.Org (2020-09-09). "Lilly Platt: Meet Earth.Org's First Global Ambassador!". Earth.Org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ "World Oceans Day Italy | World Oceans Day Online Portal". unworldoceansday.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-01. Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ "Lilly Platt Archives | Your Mark On The World". Your Mark On The World (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-20. Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ Megan Herbert (2018-11-16). "5 things I learned from a 10-year-old climate activist". Medium (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- 1 2 3 4 5 "This 11-Year-Old Activist Has Picked Up More Than 100,000 Pieces of Plastic". Global Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ "Climate change: 7 young climate activists from around the world", BBC Newsround (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2019-09-20, iliwekwa mnamo 2025-10-07
- ↑ Gemma Chandler (2018-02-23). "Lilly's Plastic Pickup mission". National Geographic Kids (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
- ↑ B. S. N. Communications (2019-08-27). "11 year old Environmentalist Taking Action (and how you can too!) | Lilly Platt | TEDxYOUTH@BSN SPEAKER". BSN Voices (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lilly Platt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |