Mnara wa taa wa Aleksandria
Mandhari
(Elekezwa kutoka Lighthouse of Alexandria)
Mnara wa taa wa Aleksandria (pia hujulikana kama Pharos ya Aleksandria) ulikuwa mnara wa taa mjini Aleksandria huko Misri ambao ulihesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia. Kimo chake hakijulikani kikamilifu lakini kilikuwa kati ya mita 110 na 150.
Mnara huo ulijengwa kwenye kisiwa kidogo kilichoitwa "Pharos" kilichokuwa mita chache mbele ya mwambao wa Aleksandria. Baadae mnara uliitwa kwa jina la kisiwa.
Ujenzi ulitokea wakati wa utawala wa Ptolemaio II Filadelfo (280-247 KK)[1] ambapo unakadiriwa kuwa angalau ni mita 100 za urefu wa jumla.[2]. Kwa karne nyingi Pharos ilikuwa kati ya majengo marefu ya dunia. Iliporomoka baada ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea Aleksandria miaka 1303 na 1323.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Picha ya Pharos kwenye sarafu za Aleskandria zilizotolewa wakati wa Dola la Roma.
-
Mnara wa Aleksandria
-
Mnara wa taa wa Alexandria
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Clayton, Peter A. (2013). "Chapter 7: The Pharos at Alexandria". Katika Peter A. Clayton; Martin J. Price (whr.). The Seven Wonders of the Ancient World. London: Routledge. uk. 11. ISBN 9781135629281.
- ↑ Clayton, Peter A. (2013). "Chapter 7: The Pharos at Alexandria". Katika Peter A. Clayton; Martin J. Price (whr.). The Seven Wonders of the Ancient World. London: Routledge. uk. 147. ISBN 9781135629281.
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mnara wa taa wa Aleksandria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |