Levan Gabriadze
Levan "Leo" Gabriadze (alizaliwa 6 Novemba 1969) ni muigizaji na mkurugenzi wa filamu wa Georgia na Urusi.
Anajulikana zaidi kwa kuongoza filamu ya kutisha ya 2014 ya Unfriended.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Gabriadze alizaliwa Tbilisi, wakati huo ikiwa sehemu ya Georgia ya Kisovyeti. Baba yake, Revaz Gabriadze, alikuwa muigizaji, mwandishi na mkurugenzi. Kufikia umri wa miaka 12, Leo tayari alikuwa akifanya kazi katika maonesho ya baba yake.
Akiwa na umri wa miaka 17, alialikwa kuigiza katika moja ya nafasi kuu kwenye filamu Kin-dza-dza!. Alihitimu kutoka katika warsha ya Shota Rustaveli Theatre and Film University, akibobea katika uigizaji na usanifu wa jukwaa.[1] Alihudumu katika Jeshi la Kisovyeti, Vikosi vya Ulinzi wa Anga akiwa na cheo cha praiyvate, akihudumu kama zima-moto.[2] Mwaka 1990, alijiunga na Chuo Kikuu cha California (UCLA) (Los Angeles) katika Kitivo cha Usanifu na Uhuishaji. Mwaka 2000, alihamia Moscow, ambako alikua mkurugenzi wa matangazo wa kampuni ya filamu Bazelevs.[3]
Mnamo mwaka 2010, alitengeneza filamu yake ya kwanza Lucky Trouble ambayo ilishinda tuzo ya watazamaji "Golden Taiga" kwenye tamasha la "Spirit of Fire" lililofanyika Khanty-Mansiysk Februari 2011.[4][5]
Mnamo mwaka 2014, aliongoza filamu ya kutisha Unfriended.[6][7][8] Mnamo mwaka 2017, alikamilisha kazi ya filamu ya uhuishaji iliyotokana na hadithi za baba yake Rezo Gabriadze, iitwayo Rezo. Filamu hiyo ilitolewa Mei 2018
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Levan Gabriadze" (kwa Russian). Time Out.
{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Lep Gabriadze" (kwa Russian). Sostav.ru.
{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "GABRIADZE Levan". kinoglaz.fr.
- ↑ ""Сибирь…" отмечена "Золотой тайгой"" (kwa Russian). Ruskino. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Фильм "Выкрутасы" дал старт "Российским дебютам" фестиваля "Дух огня"". RIA Novosti. 20 Februari 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Dave McNary (16 Oktoba 2014). "Universal Buys, Sets April Release for Blumhouse Horror-Thriller 'Cybernatural'". Variety.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Elbert Wyche. "Timur Bekmambetov, 'Unfriended'". Screen International.
- ↑ Timur Bekmambetov (11 Aprili 2015). "In 'Unfriended,' horror comes to life online". Los Angeles Times.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Levan Gabriadze kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |