Nenda kwa yaliyomo

Levan Aghniashvili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Levan Aghniashvili (1897-1937) alikuwa wakili wa Georgia na Profesa wa Sheria ambaye alihudumu kama Rector wa saba wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Tbilisi katika kipindi cha kati ya Aprili 1933 na Julai 1935.

Baada ya kupinga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Georgia, alifukuzwa uhamishoni mnamo mwaka 1918. Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Aghniashvili alihusika katika shughuli za kisiasa nchini Ukraine, Kaukazi ya Kaskazini, na katika maeneo ya Kazan na Minsk. Kati ya mwaka 1923 na 1925, Aghniashvili alihudumu kama Mwakilishi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti nchini Ujerumani. Kuanzia mwaka 1926, alianza kutoa mihadhara katika Chuo Kikuu cha Jimbo kilichoko Tbilisi, hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo mnamo mwaka 1933.

Levan Aghniashvili alipigwa risasi na kuuawa na Wakomunisti mnamo mwaka 1937, mwaka wa ukandamizaji mkubwa. Aghniashvili alifuatwa na Karlo Oragvelidze ambaye pia alikuwa mhanga wa ukandamizaji wa Wakomunisti, na yeye pia alipigwa risasi mnamo mwaka 1937, licha ya kuwa mfuasi mkubwa wa ukomunisti na kumkosoa mwanahistoria Ivane Javakhishvili. Uongozi wa Aghniashvili katika chuo kikuu bado unakumbukwa kuwa wa muhimu, kwani Ndani ya kipindi chake ndipo Taasisi ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu ilianzishwa.

    Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Levan Aghniashvili kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.