Letesenbet Gidey
Mandhari
Letesenbet Gidey (kitigrinya: ለተሰንበት ግደይ, amezaliwa 20 Machi 1998)[1][2] ni mkimbiaji wa mbio ndefu wa Ethiopia. Mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki ya Tokyo 2020 mita 10,000, alishinda medali ya fedha katika umbali wa mashindano ya Dunia ya 2019. Letesenbet anashikilia rekodi za sasa za dunia za mita 5000 na mita 10,000, ambazo aliweka Oktoba 2020 na Juni 2021 mtawalia. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza tangu Ingrid Kristiansen kutoka 1986-1993 kushikilia rekodi zote mbili kwa wakati mmoja.[3][4] Pia anashikilia rekodi za dunia katika mbio za nusu marathon[5][6] na kukimbia kwa kilomita 15.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Doha 2019" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-10-30. Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ "Letesenbet GIDEY | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ "Gidey breaks 10,000m world record in Hengelo | REPORT | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ "Letesenbet Gidey breaks two-day-old 10,000m world record in super spikes". the Guardian (kwa Kiingereza). 2021-06-08. Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ "Letesenbet Gidey: Ethiopian breaks half marathon world record in Valencia". Sky Sports (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ Taylor Dutch (2021-10-25). "Letesenbet Gidey Shatters the Half Marathon World Record in Valencia". Runner's World (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.