Leopoldo Girelli
Mandhari
Leopoldo Girelli (alizaliwa Predore, wilaya ya Bergamo, Italia, 13 Machi 1953) ni askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Italia anayehudumu kama balozi wa Papa (nuncio) nchini India na Nepal. Aliwahi kuwa nuncio wa Israeli na Kupro, pamoja na mjumbe wa kitume kwa Yerusalemu na Palestina kuanzia 2017 hadi 2021. Amefanya kazi katika huduma ya kidiplomasia ya Vatikani tangu mwaka 1987 na hapo awali alihudumu kama nuncio wa Indonesia, Timor Mashariki, na Singapuri.[1]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Girelli alipadrishwa tarehe 17 Juni 1978 na kuingizwa rasmi katika dayosisi ya Bergamo. Alihitimu katika masomo ya teolojia. Ili kujiandaa kwa huduma ya kidiplomasia, alikamilisha masomo yake katika Chuo cha Kikanisa cha Kipapa (Pontifical Ecclesiastical Academy) mnamo 1984.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Pontificia Accademia Ecclesiastica, Ex-alunni 1950 – 1999" (kwa Kiitaliano). Pontifical Ecclesiastical Academy. Iliwekwa mnamo 19 Julai 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ (in it) Rinunce e Nomine, 12.04.2006 (Press release). Holy See Press Office. 13 April 2006. http://press.vatican.va/content/salastampa/it/bollettino/pubblico/2006/04/13/0186/00547.html. Retrieved 19 July 2019.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |