Leon Schuster

Leon Ernest "Schucks" Schuster (alizaliwa 1951) ni mtayarishaji wa filamu, mwigizaji, mchekeshaji na mwimbaji kutoka Afrika Kusini[1].
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Schuster alivutiwa na mchakato wa utayarishaji wa filamu akiwa na umri mdogo. Akiwa mtoto, yeye na kaka yake walikuwa wakifanya mizaha kuhusu familia yao na kuwarekodi. Alielezea, katika mahojiano ya mwaka 2010, kuhusu maisha yake ya awali huko Bloemfontein, "Nakumbuka nikikimbia kwenye ukumbi wa Ritz Theatre, nikicheza cowboys na wahalifu, jambo ambalo lilikuwa la kawaida sana wakati huo. Pia nakumbuka nikiwapenda Laurel na Hardy, Charlie Chaplin na Three Stooges. Siku zote nilikuwa nikiigiza mambo, na kufanya mizaha. Nilikuwa nikimdanganya bibi yangu afikirie kwamba nilijipiga risasi mguuni kwa bunduki yangu ya ya sisasi ndogo… mchuzi wa nyanya kila mahali, mimi nikilia kama nguruwe mwitu. Kufanya mizaha ni katika asili yangu tu, lakini sikuwahi kufikiria ningekuwa nyota wa filamu… hapana, mimi si nyota wa filamu, mimi ni mtu wa kawaida tu anayependa kuwaburudisha watu."[2]
Schuster alisomea Shahada ya Awali ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha Orange Free State, ambapo alicheza raga kwa timu ya kwanza. Alirudi kwa Jim Fouché kama mwalimu kwa miaka miwili.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Schuster alianza kufanya kazi katika Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini. Wakati wa kipindi chake katika shirika hilo, aliunda kipindi cha redio cha Kiafrikana cha Vrypostige[4] Mikrofoon[5] na Fanus Rautenbach - ambacho kilihusisha kuficha sauti yake[6] na kuwachezea waathiriwa wasio na hatia kwa njia ya simu.
Filamu ya kwanza ya Schuster, You Must Be Joking!,[7] ilichotayarishwa kwa ushirikiano na Johan Scholtz na Elmo de Witt, ilipata umaarufu miongoni mwa watazamaji wa Afrika Kusini na kusababisha filamu inayofuata ya You Must be Joking! Too.[8]
Mtindo wa vichekesho
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2018, mchekeshaji huyo "hakuomba msamaha kuhusu kuchezea kila aina ya dhana za kibaguzi katika filamu zake", lakini alikiri waziwazi kwamba "ana majuto kuhusu kufaidika na matumizi ya kupaka rangi ya Ngozi nyeusi". Aliendelea kusema: "Samahani sana kwamba siwezi kutengeneza Mama Jack 2. Kama ndoto ingetimia, filamu yangu inayofuata ingekuwa Mama Jack 2. Lakini haswa kwenye Twitter walisema kaa mbali na matumizi ya blackface, hayakubaliki. Walikuwa watu wa rangi nyeusi wakizungumza nami na lazima uwasikilize. Siwezi kufanya hivyo kwa sababu nitakosolewa sana. Zamani haikumsumbua mtu yeyote. Lakini sasa sitafanya blackface, siwezi kufanya hivyo. Hakuna mwigizaji hata mmoja duniani atakayefanya hivyo. Ni ubaguzi wa rangi tu".[9]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ www.imdb.com https://www.imdb.com/name/nm0776856/. Iliwekwa mnamo 2026-04-03.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help) - ↑ "A perfect prankster", Get It Online Bloemfontein (kwa American English), 2010-06-28, iliwekwa mnamo 2026-04-03
- ↑ "10 Things You Didn't Know About Leon Schuster". 10 Things You Didn’t Know About Leon Schuster (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-04-03.[dead link]
- ↑ "Die Vrypostige Mikrofoon - Vol.1 — Leon Schuster". Last.fm (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-04-03.
- ↑ https://echosrecordbar.co.za/product/55141-leon-schuster-vrypostige-mikrofoon-vol1-cd
- ↑ Drum: A Magazine of Africa for Africa (kwa Kiingereza). African Drum Publications. 2002-11.
{{cite book}}: Check date values in:|date=(help) - ↑ www.imdb.com https://www.imdb.com/title/tt0092267/. Iliwekwa mnamo 2026-04-03.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help) - ↑ www.imdb.com https://www.imdb.com/title/tt2825292/. Iliwekwa mnamo 2026-04-03.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help) - ↑ Herman Eloff. "UPDATE: Producer André Scholtz on decision to remove Schuster films: 'I was shocked, but not entirely surprised'". News24 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-03.