Lenny Kravitz

Leonard Albert Kravitz (amezaliwa Mei 26, 1964) ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Kravitz alitoa albamu yake ya kwanza, Let Love Rule mwaka 1989. Huu ulikuwa mwanzo mzuri wa kazi yake ya muziki inayojulikana kwa mchanganyiko wa mitindo mbalimbali kama rock, funk, reggae, hard rock, soul, na R&B.
Kravitz ameweza kutoa nyimbo maarufu zilizopata mafanikio makubwa, zikiwemo "It Ain't Over 'til It's Over" (1991) na "Again" (2000), ambazo zote zilifika katika 10 bora katika chati ya Billboard Top 100. Nyimbo nyingine mashuhuri ni pamoja na "Let Love Rule" (1989), "Always on the Run" (1991), "Are You Gonna Go My Way" (1993), "Fly Away" (1998), na "American Woman" (1999), ambazo pia zilifika 10 bora katika chati ya Alternative Airplay.
Kravitz ameshinda tuzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Grammy Award ya Utumbuizaji Bora wa Muziki wa Rock kwa Mwimbaji wa Kiume, ambayo aliipata kwa miaka minne mfululizo kuanzia 1999 hadi 2002,[1] akivunja rekodi ya ushindi mwingi zaidi katika kipengele hicho, na kuweka rekodi ya ushindi wa mfululizo kwa msanii wa kiume katika kipengele kimoja. Kravitz ameuza zaidi ya nakala milioni 40 ya albamu yake duniani kote na aliorodheshwa nafasi ya 93 katika orodha ya VH1 ya "Wasanii 100 Bora wa Hard Rock".[2]
Mbali na kazi yake ya muziki, Kravitz pia ameigiza katika filamu kama Precious (2009) na sehemu mbili za mwanzo za mfululizo wa filamu za The Hunger Games (2012–13). Aidha, yeye ni mwanzilishi wa studio ya ubunifu iitwayo Kravitz Design Inc. Kravitz aliwahi kumwoa Lisa Bonet, na wana mtoto wa kike pamoja, Zoë Kravitz.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "GRAMMY Award Results for Lenny Kravitz". Grammy.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 13, 2020. Iliwekwa mnamo Desemba 23, 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "VH1 100 Greatest Artists of Hard Rock". YouTube. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 21, 2017. Iliwekwa mnamo Septemba 13, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)