Leniolisib
| Data ya kikliniki | |
|---|---|
| Majina ya kibiashara | Joenja |
| Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
| Kategoria ya ujauzito | Huenda ikasababisha madhara[1] |
| Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo[1] |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Visawe | CDZ173 |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | C21H25F3N6O2 |
| |
Leniolisib, inayouzwa kwa jina la chapa Joenja, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa kuchochewa kwa kimeng'enya cha PI3K-delta (phosphoinositide 3-kinase delta (APDS)).[1] Inatumika kwa watu wenye umri wa angalau miaka 12[1] na inamezwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, maambukizi ya sinusi (sinusitis), na ugonjwa wa mzio wa ngozi (atopic dermatitis).[1] Matumizi yake wakati wa ujauzito au kunyonyesha yanaweza kumdhuru mtoto.[1] Dawa hii haipaswi kutumika kwa watu wenye matatizo makubwa ya ini.[1] Ni kizuizi cha vimeng'enya vya kuwasha mawasiliano ndani ya seli (kinase).[1]
Leniolisib iliidhinishwa kwa matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2023.[1] Ilipata cheo cha dawa yatima barani Ulaya mnamo 2020.[2] Nchini Marekani, iligharimu takriban dola za Marekani 550,000 kwa mwaka kufikia mwaka wa 2023.[3] Ni dawa ya kwanza ya APDS.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 "Joenja- leniolisib tablet, film coated". DailyMed. 29 Machi 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "EU/3/20/2339". European Medicines Agency (kwa Kiingereza). 12 Februari 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 22 Juni 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Leniolisib Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". www.goodrx.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 22 Juni 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)