Laurent Clerc
Laurent Clerc (matamshi ya Kifaransa: [lɔʁɑ̃ klɛʁ]; 26 Desemba 1785 – 18 Julai 1869 alikuwa mwalimu mwenye asili ya Ufaransa aliyejulikana kama "Mtume wa Viziwi Amerika" na anachukuliwa kuwa mtu mwenye ulemavu wa kusikia maarufu zaidi katika historia ya viziwi Amerika.
Alifundishwa na Abbé Sicard na mwalimu anayefundisha watu wenye ulemavu wa kusikia Jean Massieu, katika Taasisi ya Kitaifa ya watu wenye ulemevu wa kusikia na kuongea Paris. Pamoja na Thomas Hopkins Gallaudet, walianzisha shule ya kwanza ya wenye ulemavu wa kusikia Amerika Kaskazini, yaani Asylum for the Education and Instruction of the Deaf and Dumb, tarehe 15 Aprili 1817, katika hoteli ya zamani ya Bennet's City Hotel, Hartford, Connecticut. Shule hiyo baadaye iliitwa American School for the Deaf na mwaka 1821 ilihamia 139 Main Street, West Hartford. Shule hiyo ipo bado na ni shule kongwe zaidi ya viziwi iliyopo Amerika Kaskazini.