Nenda kwa yaliyomo

Laurean Rugambwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Laurean Rugambwa (12 Julai 1912 - 8 Desemba 1997) alikuwa askofu Mkatoliki nchini Tanzania aliyeendelea na kuwa kardinali wa kwanza kutoka Kusini kwa Sahara katika Kanisa Katoliki.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Bukongo-Kamachumu (Bukoba) tarehe 12 Julai 1912 akapewa upadri tarehe 12 Desemba 1943.

Tarehe 13 Desemba 1951 aliteuliwa kuwa askofu na Vikarieti ya Kitume ya Kagera kusini. Alipewa daraja takatifu hiyo tarehe 10 Februari 1952 na askofu David Mathew. Eneo alilokabidhiwa likafanywa kuwa jimbo la Rutabo tarehe 25 Machi 1953 na tarehe 21 Juni 1960 likabadilishiwa jina kuwa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Papa Yohane XXIII alimteua kuwa kardinali tarehe 28 Machi 1960 akimkabidhi usimamizi wa parokia ya San Francesco d'Assisi a Ripa Grande mjini Roma. Alikuwa kardinali wa kwanza asiye Mzungu.

Tarehe 19 Desemba 1968 alihamishiwa kwenye jimbo kuu la Dar-es-Salaam aliloliongoza hadi alipojiuzulu kutokana na uzee tarehe 22 Julai 1992.

Alishiriki Mtaguso wa pili wa Vatikano, na mikutano mitatu ya uchaguzi wa Papa (1963, 1978 na 1978 tena).

Alifariki mjini Dar es Salaam tarehe 8 Desemba 1997 akiwa na umri wa miaka 85.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.