Nenda kwa yaliyomo

Laura Marholm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Laura Katharina Marholm

Laura Katharina Marholm (18541928) alikuwa mwandishi wa Kibatiki-Kijerumani aliyeandika ukaguzi wa fasihi, wasifu wa wanawake, na riwaya. Wahusika wakuu katika riwaya zake walikuwa wanawake waliokuwa na furaha na kuridhika katika ndoa. Marholm alikuwa mwanamke wa kisasa wa harakati za kike (New Woman feminist) ambaye aliandika kuhusu masuala ya ukombozi wa wanawake. Kutokana na baadhi ya imani zake, baadhi ya wanamke wengine wa harakati za kike hawakumuona Marholm kuwa mmoja wao. Alikuwa na imani kwamba fasihi inaweza kutumika kusaidia katika uhusiano kati ya jinsia. Baadhi ya kazi za Marholm zilihesabiwa kama sehemu ya "ukaguzi wa fasihi wa kike" (gynocriticism), miaka 70 kabla ya neno hilo kuanzishwa rasmi, ambapo sehemu kubwa ya kazi hiyo ilikuwa ikizingatia waandishi wanawake wa Nordic.[1]

  1. Sjöblad, Christian (3 Agosti 2018). "Laura Katharina Marholm". Svenskt kvinnobiografiskt lexikon. Iliwekwa mnamo 12 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Laura Marholm kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.