Latitudo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya dunia inayoonyesha mistari ya longitudo na latitudo.

Latitudo (kwa Kilatini: latitudo) ni mahala pa mchoro wa dunia au ramani huonyesha kwa mistari iliolazwa ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka ikweta kwa kipimo cha digrii (°).

Mahali penye ikweta kamili (kwa mfano Nanyuki katika Kenya) ina latitudo ya "0". Mahali pa mbali ni ncha ya kaskazini au ya kusini zinazotajwa kwa 90°. Pamoja na kipimo cha longitudo inataja mahali kamili duniani.

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north) na "S" (south) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Digrii za latitudo hugawiwa katika umbali wa 60 dakika au minuti; dakika ya latitudo ni mita 1852 au maili moja ya kibahari. Dakika hugawiwa katika nukta au sekondi. Mfano: 13°19.717′ N.

Latitudo muhimu ni:

1. Ikweta (0°)

2. Tropiki ya kansa (23½°Kas)

3. Tropiki ya kaprikoni (23½°Kus)

4. Duara la aktiki (66½°Kas)

5. Duara la antaktika (66½°Kus)

Pamoja na namba ya longitudo inaonyesha mahali kamili kwenye uso wa dunia.