Nenda kwa yaliyomo

Latifa Baka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Latifa Baka (alizaliwa 1964) ni mwandishi na mwanahabari kutoka nchini Moroko, ni mwandishi wa riwaya na hadithi fupi . [1]

Anafundisha sosholojia huko Agadir . [2]

Maisha na Kazi

[hariri | hariri chanzo]

Latifa Baka alizaliwa mjini Casablanca. Alianza kujipatia umaarufu katika miaka ya 1990 kupitia maandishi yake yaliyochapishwa katika magazeti na majarida ya kitamaduni nchini Moroko.

Kazi yake muhimu zaidi ilikuwa mkusanyiko wa hadithi fupi uitwao "Depuis ce temps-là" (Tangu wakati huo) uliochapishwa mwaka 1992, ambao ulimfanya ashinde tuzo ya kifasihi ya "Prix du Maroc" katika kundi la waandishi vijana[3].

Baadaye aliandika riwaya kadhaa ikiwa ni pamoja na since this life and room of Virginia Wolff (tangu maisha haya na chumba cha Virginia Wolff). Kupitia maandishi yake, mwandishi anatoa maelezo wazi ya vikwazo katika jamii ya Morocco na vikwazo vya maendeleo ya wanawake. Kazi zake ziliwasilishwa kama sehemu ya toleo la tisa la Tamasha la Kimataifa la Filamu la Wanawake huko Salé, mnamo 2015. [4] [5]

Kazi Mashuhuri

[hariri | hariri chanzo]
  • Depuis ce temps-là (1992) – Mkusanyiko wa hadithi fupi.
  • De quel amour blessé (2003) – Riwaya.
  • Ameshiriki katika mkusanyiko wa kazi za pamoja kama vile "Femmes et écriture au Maroc" (Wanawake na Uandishi nchini Moroko).
  1. Salim Jay, Dictionnaire des écrivains marocains, Casablanca: Eddif, 2005, pp. 58-59
  2. Jay, Salim (2005). Dictionnaire des ecrivains marocains. Internet Archive. Casablanca : Eddif ; Paris : Paris-Mediterranee. ISBN 978-9981-09-111-5.
  3. "Latifa Baqa". bladinet (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2026-01-24.
  4. Khalil, Andrea (2013-10-18). North African Cinema in a Global Context: Through the Lens of Diaspora (kwa Kiingereza). Routledge. ISBN 978-1-317-96863-4.
  5. MATIN, LE (2004-07-03). "Festival International du Film de Salé : «Ecrans de femmes»". Le Matin.ma (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-02-01.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Latifa Baka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.