Lata Mangeshkar
Lata Deenanath Mangeshkar (alizaliwa Hemalata Deenanath Mangeshkar; 28 Septemba 1929 – 6 Februari 2022) alikuwa mwimbaji wa Uhindi wa kurekodi sauti za filamu (playback singer) na mtunzi wa muziki wa mara kwa mara. Anachukuliwa kuwa mmoja wa waimbaji wakuu na wenye ushawishi mkubwa zaidi katika rasi ya India. Mchango wake katika tasnia ya muziki wa India katika kazi yake iliyodumu kwa miongo minane ulimletea vyeo vya heshima kama vile 'Malkia wa Melodi' na 'Sauti ya Milenia. [1][2][3]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Mangeshkar alizaliwa tarehe 28 Septemba 1929 huko Indore (katika wilaya ya sasa ya Indore mkoani Madhya Pradesh), ambayo wakati huo ilikuwa mji mkuu wa jimbo la kifalme la Indore lililokuwa sehemu ya Mamlaka ya India ya Kati katika utawala wa kikoloni wa Uingereza (British India).[4][5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1942, Mangeshkar akiwa na umri wa miaka 13, baba yake alifariki kwa ugonjwa wa moyo. Master Vinayak (Vinayak Damodar Karnataki), mmiliki wa kampuni ya filamu ya Navyug Chitrapat na rafiki wa karibu wa familia ya Mangeshkar, alichukua jukumu la kuwatunza. Alimsaidia kuanza kazi yake ya sanaa kama mwimbaji na mwigizaji.[6][7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nytimes.com/2022/02/05/world/asia/lata-mangeshkar-dead.html
- ↑ https://www.economist.com/obituary/lata-mangeshkar-was-the-soundtrack-of-the-newly-independent-country/21807600
- ↑ https://archive.org/details/insearchoflatama00bhim/page/54/mode/2up?q=Yesubai
- ↑ https://timesofindia.indiatimes.com/articleshow/30899862.cms
- ↑ https://www.hindustantimes.com/inspiring-lives/lata-mangeshkar-the-queen-of-melody/story-TBN6Pq9c9wktF7ptW0gBmN.html
- ↑ https://web.archive.org/web/20041103120451/http://www.hindu.com/lf/2004/09/21/stories/2004092114010200.htm
- ↑ https://www.bbc.com/news/world-asia-india-60257952
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lata Mangeshkar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |