Lango:Kenya/Wasifu uliochaguliwa/5

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jomo Kenyatta

Jomo Kenyatta (1893-1978) alikuwa rais wa kwanza wa Kenya, alizaliwa mwaka 1893 jina lake halisi ni Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata. Kabila lake lilikuwa ni Mgĩkũyũ. Alisoma katika shule ya kanisa la wamisheni wa Kiskoti.

Baada ya kuhitimu aliajiriwa kama karani na msoma mita wa manispaa ya Nairobi, alioa mke wake wa kwanza ambaye ni Grace Wahu.

Azma yake ya kutaka kuikomboa ardhi ya Wagĩkũyũ ilimfanya kuweza kuwaunganisha Wagĩkũyũ naye akawa katibu wao mwaka 1928.

(Soma Zaidi...)