Lango:Historia/Intro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wa wakati uliopita. Mara nyingi neno historia pia lina maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").

Wanahistoria wanapata maarifa zao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa Historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa Historia ya awali).